
Akizungumza kabla ya kuanza kuchangia muswada wa sheria ya fedha ya mwaka 2013/2014, Waziri kivuli wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi wa Chadema, Halima Mdee alisema, “Kabla sijaanza kuchangia Mheshimiwa Spika naomba nianze kwa kuwapa pole wakazi wote wa Arusha kutokana na mlipuko wa bomu uliosababisha watu kupoteza maisha, kwani tangu limetokea tukio hilo leo ndiyo nazungumza kwa mara ya kwanza,” “Tunazilaani kauli potofu zilizotolewa na Serikali hapa bungeni, Serikali inajua nini kilichotokea Arusha na ilitumia kutokuwepo kwetu kupotosha,” alisema.
Source: Butahe F. (June 2013).Chadema wamjibu Waziri Mkuu. Dodoma. Retrieved from Mwananchi
No comments:
Post a Comment