Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Wednesday, May 29, 2013

Wazee wailaani CCM


    WAZEE wa Kata ya Ng’ang’ange, wilayani Kilolo, Iringa wamelaani mfumo wa uongozi uliopo na kuwaongoza baadhi ya wananchi kurudisha kadi za Chama Cha Mapinduzi (CCM). Hayo yalitokea juzi katika kata hiyo wakati wa kampeni za kumnadi mgombea wa udiwani kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambapo zaidi ya wanachama 250 walirudisha kadi za CCM na kujiunga na CHADEMA. Wakiongozwa na mzee Lucian Mahenge (74) kurudisha kadi hizo, alisema hakuna sababu ya kuendelea kuking’ang’ania chama kisicho na msaada na kwamba hakina jipya.

     “Baada ya miaka mingi ndani ya CCM nimeona kuna mateso na si uhuru tena tulioahidiwa. Uhuru alioutafuta Baba wa Taifa umegeuka kuwa mateso kwetu sasa najiuliza imekuwa hivi kwa sababu Baba wa Taifa hayupo tena duniani? “Nawaomba wazee wengu, wanaume na wanawake tuungane na vijana wetu kuhakikisha mateso haya tunayakimbia ndani ya CCM,” alisema Mahenge. Alisema kumekuwa na ubaguzi uliopindukia katika utoaji huduma hali inayosababisha watu kupata tabu na kutokujua hatima ya maisha yao. “Ndugu zangu, mimi mzee wenu ambaye tangu uhuru nipo ndani ya CCM nawaambia ukweli kuwa CCM ya Baba wa Taifa siyo hii mnayoiona leo. Huu ni mzoga. CCM ya wakati huo ilikuwa ni nzuri, nimefikiri sana nikaona chama kinachoweza kutusaidia kwa sasa ni CHADEMA. Tuungane kwa pamoja tuiage CCM iliyooza,” alisema.

      Naye Mratibu wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Frank Mwaisume, akimnadi mgombea udiwani alisema miaka 50 baada ya Uhuru Watanzania bado ni wachovu na kwamba hakuna matumaini ya kupata ahueni kupitia serikali iliyopo madarakani. Naye mgombea udiwani kwa tiketi ya CHADEMA, Nafred Lucas Chahe, aliwataka wananchi wa kata hiyo kumfanya kuwa daraja ili awatumikie kwa dhati, ili maendeleo yapatikane. “Tuna mambo mengi sana hapa kwetu hayajawahi kutatuliwa miaka 50 iliyopita hadi leo. Mnifanye kuwa msemaji wa mambo haya ili yaweze kutatuliwa.

    “Malengo yetu tunayopanga yatatimia tukishirikiana kwa pamoja ila cha msingi ni kunipa kura yenu ili niweze kuwa diwani wenu,” alisema. Mkutano huo ulikwenda sambamba na ufunguzi wa ofisi ya kata ambayo imejengwa kwa jitihada za mgombea udiwani huyo.

Source: Chache G. (May 2013). Wazee wailaani CCM. Kilolo. Retrieved from Tanzania Daima

No comments: