Sasa ni wazi kwamba aliyekuwa kamanda wa
Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza ameuawa na genge ndani ya Polisi akiwemo Kamanda
Polisi anayejulikana kwa jina la Muna, gazeti la Jamhuri limeripoti katika
ukurasa wa Mbele kabisa (Nimesoma kwenye website yao Deo Balile akilalamika
gazeti kununuliwa kwa jumla na watu wasiojulikana)
Kuvuja kwa siri hiyo kumetokana na mmoja
wa jambazi sugu ajulikanaye kwa jina la Edward Malele kujisalimisha ktk vyombo
vya ulinzi na kutoa siri zote. Jambazi huyu aliombwa wa genge ndani ya
polisi kushiriki katika mpango wa kumwua kamanda Barlow. Akakataa kwa kuwa
aliwahi kumfahamu kwa karibu kamanda Barlow. Baada ya kukataa kutekeleza agizo hilo
baada ya siku chache alishtakiwa kwa kosa la ujambazi na kuswekwa Rumande.
Akiwa huko ndani ya wiki moja alisikia
habari za kifo cha kamanda Barlow. Akajua akina na Muna aliowakatalia wamefanya
kazi aliyoikataa yeye. Na alijua yuko mahabusu kwa sababu ya kukataa mradi huo. Baada ya kukaa huko muda mrefu bila
shitaka kueleweka wala mshataki wake huko Lupango walimua kumwaichia. Akagoma
kutoka kwa sababu anajua kuwa, kwa kuwa amepelekwa huko ili kuficha siri hivyo,
akitoka lazima atauawa. Baada ya muda akaamua kukubali kutoka lupango na
kukimbilia kituo cha JWTZ huko Mwanza.
Huko JWTZ Alijieleza vya kutosha na wanajeshi
walimwonea huruma wakampa Nauli na Tsh 10,000/= ya kula njiani ilie aende
Bungeni huku wakiwa wamemkabidhi namba za simu za wabunge 2 wa upinzani ili
wamsaidie. Kutokana na kutokuelewa kwake alipokuwa
anashangaa shangaa katika eneo la Bunge, alikamatwa na polisi wanalinda eneo
hilo. Polisi hao wakapiga simu Dodoma central na Mwanza. Haraka haraka mwanza
wakataka arudishwe mwanza kwa kuwa ni jambazi sugu.
Hata hivyo, kwa katika kurupushani hiyo
taarifa zimeshameshamfikia Pinda na Nchimbi ambapo gazeti linaripoti kuwa Pinda
ameagiza kijana huyo apewe ulinzi na asirudishwe Mwanza. Hata hivyo amepelekwa kusiko
julikana. Kwa mapana zaidi soma gazeti la Jamhuri
KAMA zinanunuliwa kwa kasi na watu wasiofahamika.
My take;
CCM inaua waandishi na polisi ambao
imetofautiana nao. Huo ndio ukweli, watake wasitake. CCM ni janga la kitaifa.
na Imeshindwa kuongoza nchi.
From this generation Bilionea.
Source: Obe B. (May 2013). Siri za kifo cha Kamanda Barlow zavuja, kamanda wa Polisi Muna atajwa! Taarifa zamfikia Pinda. Retrieved from Jami Forums

No comments:
Post a Comment