Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Friday, May 17, 2013

Mchakato wa Katiba kufikishwa mahakamani Jumatatu


Jukwaa la Katiba Tanzania, limesema limekamilisha mchakato wa kwenda mahakama Kuu na Mei 20, mwaka huu watatinga mahakamani. Jukwaa hilo linakwenda Mahakamani kuweka zuio dhidi ya Tume ya Marekebisho ya Katiba, kusitisha mchakato wa Katiba mpya hadi watakaporekebisha kasoro zilizojitokeza. Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, akizungumza na NIPASHE jana, Deus Kibamba, alisema wamefanya vikao kadhaa na jopo la mawakili 10 ambao wanaendelea kuandaa hoja za msingi. “Tumeshafanya vikao kadhaa na jopo la Mawakili wakiongozwa na Mwanasheria wa masuala ya Haki za Binadamu, Dk. Rugemeleza Nshala, wamefika pazuri na Jumatatu tutakuwa mahakamani,” alisema Kibamba. Kibamba alisema uamuzi wakwenda mahakamani unatokana na Jukwaa hilo kupuuzwa na mihimili ya Bunge na Serikali na wasaidizi wa Rais kuwakataza kuonana na Rais, Jakaya Kikwete, kwa ajili ya kuwasilisha maoni yao na kuona njia pekee ya kutafuta haki ya Watanzania ni kwenda mahakamani.

“Tunaenda mahakamani kuomba isimamishe mchakato wa Katiba mpya hadi watakaoona umuhimu wa kuheshimu na kufuata ratiba waliojiwekea, kuheshimu misingi ya uandikaji na iamuru kusimama kwa mchakato huo,” alisema. Alianisha kasoro ni mchakato huo kupelekwa kwa kasi inayoathiri misingi mikuu ya ujenzi wa Katiba mpya kwenye  uelewa na hamasa, ushiriki, umiliki wa wananchi na hivyo mchakato huo unaweza kuzaa Katiba isiyo na sauti na maoni ya Watanzania wote. Alisema wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya walichaguliwa kwa mizengwe, rushwa na ushabiki wa kiitikadi za vyama, dini na wengi hawana sifa muhimu za kuchambua, kutafsiri na kujadili rasimu ya katiba mpya. Alisema nyingine ni Bunge Maalum la Katiba, kutokuwa na sifa kwa kuwa ni wa kuchaguliwa na kuweka watu huru, kwa kuwa wabunge waliopo Dodoma na Zanzibar hawakuchaguliwa kwenda kutunga Katiba Mpya bali sheria za kawaida za nchi ikiwamo marekebisho ya Katiba.
 

Source: Kitomary S. (May 2013).Mchakato wa Katiba kufikishwa mahakamani Jumatatu. Retrieved from Ippmedia/Nipashe

No comments: