Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Monday, April 15, 2013

Serikali na hujuma kwa raia:Yalalamikiwa kushindwa kusaidia wakulima kuwa na maisha bora


Zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania wameajiriwa na sekta ya kilimo



Ni jambo lenye kushangaza, lakini ndio hali ilivyo kwamba Serikali inalalamikiwa kuhujumu wakulima nchini. Kambi ya Upinzani Bungeni imelia na Serikali kwa kueleza kuwa inafanya hujuma dhidi ya wakulima  wa ndani kwa kuwa mchele unaotoka nje kwa punguzo la kodi unasababisha mkulima kulazimika kuuza mpunga wake kwa bei ambayo haiwezi kukidhi gharama za uzalishaji.
Akisoma  hotuba yake bungeni Msemaji wa kambi hiyo kwa Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), David Silinde kuhusu makadirio na matumizi ya Tamisemi kwa mwaka 2013/14, alisema ni muhimu Serikali ikawaeleza wakulima ni kigezo gani inakitumia kutoa kibali vya uagizaji wa mchele huku ikielewa imekuwa ikihamasisha wakulima kulima mchele ambao uko kwa wingi. Silinde alihoji kama kuna haja ya wakulima kuendelea kulima wakati Serikali haina nia ya dhati ya kuwaondolea umaskini wakulima.
“Nchi zote duniani ambazo zimeendelea, jambo la kwanza walihakikisha na wanaendelea kuhakikisha kuwa wakulima wao wanalindwa kutokana na nguvu ya soko,” alisema Silinde na kuongeza: “Hivyo basi ni wajibu wa Serikali kuhakikisha kuwa wakulima wanalindwa kwa kutoa fidia ya tofauti ya bei ili waweze kukidhi gharama za uzalishaji na kwa njia hiyo wakulima wataendelea na kilimo na pia kulipa madeni yao kutoka taasisi mbalimbali za fedha.”
Alisema wakulima wengi hasa wa mpunga walilima na wamevuna mpunga mwingi hivyo maghala hasa katika Mikoa ya Morogoro, Mbeya na Kilimanjaro yamejaa mpunga. “Kutokana na neema hiyo mavuno ambayo imeshuka kwa wakulima, jambo la ajabu ni kwamba Serikali huku ikielewa hali halisi ya mavuno ya mpunga imetoa vibali kwa wafanyabiashara kuagiza mchele toka nje na mchele na unaingizwa kwenye soko.”
Source: Mwananchi (April 2013). Serikali na hujuma kwa raia:Yalalamikiwa kushindwa kusaidia wakulima kuwa na maisha bora. Retrieved from Mwananchi

No comments: