NIlitaka kuandika kwa kirefu lakini nimeonelea niandika kwa ufupi tu:
Mahakama itatakiwa kufutilia mbali kesi ya Lwakatare na Ludovick mara moja. Wahusika mbalimbali wa kesi hii (wengine mawakili) na potential witnesses wametumia nafasi zao (Bungeni) kuzungumzia suala la kihalifu kiasi kwamba haki haiwezi kutendeka kwa watuhumiwa. Ikumbukwe kuwa yanayozungumzwa Bungeni yana kinga na hivyo anayeyasema hawezi kuhojiwa juu yake. Mahakama imeingiliwa kuliko kiasi na wakati umefika kesi hii inatakiwa ifutwe mara moja. Na hapo hatujagusa suala la technicality za ushahidi (kama ile video ambayo bado nailia timing nzuri kuiweka hapa for "educational purposes". Mahakama ikiendelea kusikiliza kesi hii itajithibitisha kuwa haina uwezo wa kugombania uhuru wake mbele ya wanasiasa!
Mahakama inaweza vipi kuendelea na kesi ya uhalifu wakati Bunge limeshaingilia kati tena kuingilia vibaya kwa baadhi ya wabunge kuwaita watuhumiwa "Maghaidi"? na wengine wakianza kutishia potential witnesses? Isn't this tampering with the course of justice?
Mahakama itoe funzo kwa wanasiasa maana inaonekana wameanza kujisahau na kupitiliza; wao wanataka wawe watendaji, wao wanataka kuwa mahakama, na wao wanataka kuwa watunga sheria! na wakati mwingine wanataka kuwa polisi hao hao!
Mimi Mwanakijiji

No comments:
Post a Comment