![]() |
| Kamanda Alphonse Mawazo |
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), kupitia kampeni ya Movement for Change (M4C), Kanda ya Ziwa,
kimeandaa karamu ya chakula cha usiku kwa wadau, wanaharakati, wapenzi wa
chadema na wananchi wapenda maendeleo, kwa lengo la kupata michango ya fedha
zitakazowasaidia viongozi wa chama hicho vijijini.vTaarifa iliyotolewa na
kiongozi wa M4C Kanda ya Ziwa, 'Kamanda' Alfonce Mawazo ilisema hafla hiyo
itafanyika Aprili 28, mwaka huu jijini hapa na itahudhuriwa na wabunge
mbalimbali wa Chadema hicho.
"Tunatarajia kupata wageni kutoka
mikoa ya Kagera, Mara, Geita, Simiyu, Mwanza na Shinyanga ambao wote hawa ni
kutoka kanda ya ziwa…fedha tutakazokusanya zitatumika kwa ajili ya kuleta
ukombozi kwa wananchi wa Tanzania kwa kuiondoa madarakani CCM mwaka 2015,"
alisema Mawazo.v"Kwa hiyo, tunawaomba wadau, wanaharakati, wananchi, wana
CCM, wapenzi na mashabiki wa CHADEMA na wapenda maendeleo wote waje tushiriki
pamoja kufanikisha safari ya Chadema kuingia madarakani 2015", alisema
Mawazo.
Alisema CHADEMA imeandaa kadi maalumu kwa
watu wote wanaohitaji kushiriki hafla hiyo, pia alitoa wito kwa wananchi
kuwasiliana na viongozi wa Chadema, ili wapate kadi hizo kwa ajili ya kushiriki
kwenye hafla hiyo. Kuhusu mafanikio ya M4C Kanda ya Ziwa, aliwapongeza
viongozi na wanachama wa CHADEMA, kwa mshikamano mzuri wa kuongoza harakati za
mageuzi katika kanda hiyo.
Source: Matimo C. (April 2013). M4C
kuendesha harambee. Mwanza. Mtanzania

No comments:
Post a Comment