Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Wednesday, April 17, 2013

‘Kanuni zinawapa jeuri mawaziri kujibu usanii’



MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (CHADEMA) amesema kuwa mabadiliko ya kanuni mpya ya upitishaji wa bajeti yanawapa mwanya mawaziri kutoa majibu ya uongo na kisanii. Mdee alisema hayo jana wakati akiomba mwongozo wa spika, akihoji kanuni inayotumika wakati Bunge linapokaa kama Kamati ya Matumizi kupitisha vifungu vya bajeti. Alisema uzoefu aliouona juzi wakati Bunge lilipokaa kama Kamati ya Matumizi kupitia vifungu vya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2013/2014, wabunge waliohoji mambo mbalimbali ya kisera hawakupata fursa tena ya kuhoji.

"Mheshimiwa spika, hapa tuko kwenye Bunge la bajeti na uzoefu niliouona jana Bunge lilipokaa kama Kamati ya Matumizi, wabunge waliohoji hawakupata fursa ya kuuliza tena hata kama majibu ya serikali hayakuwa sahihi," alisema. Kabla ya mabadiliko hayo ya kanuni, wabunge wanaohoji walikuwa na fursa ya kuwabana mawaziri. Mdee alisema mabadiliko hayo ya kanuni yanawapa fursa mawaziri kujibu uongo na usanii kwani hawawezi tena kubanwa.

Akijibu mwongozo huo, Naibu Spika Job Ndugai alisema mabadiliko hayo ya kanuni yalipitishwa na wabunge wenyewe na kiti chake hakiwezi kubadilisha. Alisema moja ya mabadiliko yaliyofanywa kutokana na kilio cha wabunge ni kutenga dakika 25 kuwapa fursa wabunge watano kuhoji. Chini ya kanuni hiyo, wabunge watatu watatoka CCM, mmoja CHADEMA na mwingine CUF na kama kuna mbunge mwingine kutoka TLP, NCCR Mageuzi na UDP, atachukua nafasi moja ya CCM. "Hii ndiyo kanuni tuliyopitisha na imetokana na kilio chenu wenyewe. Sasa tunawapa watu kanuni waone kama kuna haja ya kufanya marekebisho?" alisema.

Source: Malera M. (April 2013). Kanuni zinawapa jeuri mawaziri kujibu usanii. Dodoma, Retrieved from Tanzania Daima

No comments: