JIBU LA SWALI LA MBUNGE VITI MAALUM
AHADI zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete wakati wa kugombea nafasi yake ya urais zimeendelea kuwatesa wabunge kwa madai mpaka sasa hazijatekelezwa na zinawapa wakati mgumu kwa wananchi. Hayo yalibainika bungeni jana baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Esther Bulaya (CCM), alipouliza swali la nyongeza na kuhoji ni lini serikali itajenga barabara ya Bunda -Kisorya ambayo ipo katika ahadi ya rais. Aidha, alitaka kujua kama fedha sh bilioni nane zilizotengwa katika ujenzi wa barabara zitatumika kwa ujenzi wa barabara ama kulipa fidia kwa watu waliopisha upanuzi wa barabara hiyo.
Katika swali la msingi, mbunge huyo alitaka kujua iwapo serikali ilishaahidi kutangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya Nyamuswa-Bunda-Kisorya, lakini mpaka sasa bado haijatangazwa. Kutokana na hali hiyo, Bulaya alitaka kujua serikali itatangaza lini zabuni hiyo ili ujenzi wa barabara hiyo uanze. Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Gerson Lwenge, alisema barabara ya Nyamuswa – Bunda – Kisorya ni kiunganishi muhimu kati ya Wilaya ya Bunda, mkoani Mara na Visiwa vya Ukerewe, mkoani Mwanza. Mhandisi Lwenge alisema zabuni ya ujenzi kwa kiwango cha lami kwa barabara ya Nyamswa - Bunda – Kisorya, sehemu ya Kisorya - Bunda yenye urefu wa kilomita 82 imetengenezwa Machi 28, mwaka jana.
Source: Tanzania Daima. (April 2013). Ahadi za JK bado zawatesa wabunge. Dodoma. Retrieved from Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment