UTANGULIZI
Kupitia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ibara 115 inatambua umuhimu na michango ya raia wa Tanzania wanaoishi nje ya nchi (Diaspora). Ilani pia inatamka kuwaekea mazingira maalum kwa raia wa Tanzania wanaoishi nje ya nchi ili waweze kuendelea kuchangia maendeleo ya Tanzania kwa urahisi zaidi. Tamko hilo la Ilani ya CCM lilipelekea Watanzania wengi wanaoishi nje ya nchi kama UK, USA, Canada na India kuanzisha matawi ya CCM katika nchi hizo wanazoishi kadhalika Watanzania hao wanaoishi nje ya nchi walijikusanya na kuanzisha Jumuiya katika nchi hizo wanazoishi kama umoja wa Watanzania wanaoishi Uingereza (TZ-UK) Umoja wa Watanzania wanaoishi Marekani (DICOTA), Umoja wa Watanzaia wanaoishi Canada na Umoja wa Watanzania wanaoishi India.
Kupitia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ibara 115 inatambua umuhimu na michango ya raia wa Tanzania wanaoishi nje ya nchi (Diaspora). Ilani pia inatamka kuwaekea mazingira maalum kwa raia wa Tanzania wanaoishi nje ya nchi ili waweze kuendelea kuchangia maendeleo ya Tanzania kwa urahisi zaidi. Tamko hilo la Ilani ya CCM lilipelekea Watanzania wengi wanaoishi nje ya nchi kama UK, USA, Canada na India kuanzisha matawi ya CCM katika nchi hizo wanazoishi kadhalika Watanzania hao wanaoishi nje ya nchi walijikusanya na kuanzisha Jumuiya katika nchi hizo wanazoishi kama umoja wa Watanzania wanaoishi Uingereza (TZ-UK) Umoja wa Watanzania wanaoishi Marekani (DICOTA), Umoja wa Watanzaia wanaoishi Canada na Umoja wa Watanzania wanaoishi India.
Majukumu ya Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
Kwa mujibu wa Katiba ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 1977, Toleo la Mei 2005. Ibara ya 117 (4) inaeleza kuwa Idara za Sekretarieti za Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa itatekeleza majukumu na kazi zake ambazo kwa upande wa Bara zinatekelezwa na Idara za Sekretarieti za Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
Kwa mujibu wa Katiba ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 1977, Toleo la Mei 2005. Ibara ya 117 (4) inaeleza kuwa Idara za Sekretarieti za Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa itatekeleza majukumu na kazi zake ambazo kwa upande wa Bara zinatekelezwa na Idara za Sekretarieti za Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
Kwa maana hiyo, kazi za Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa zitakuwa kama zilivyoorodheshwa katika Ibara ya 113 (3). Baadhi ya majukumu hayo kwa mujibu wa Ibara ya 113 (3) (b), (e), (f) na (g)
- Kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na Sera za Kijamii za CCM
- Kuratibu uhusiano na ushirikiano wa CCM na vyama vya siasa vya kidugu,kirafiki na vya kimapinduzi
- Kufuatilia hali ya kisiasa katika nchijirani na nchi nyinginezo duniani
- Kufuatilia maendeleo ya Kamati zaUrafiki na mshikamano kati yaWatanzania na wananchi wa nchirafiki.
Hatua za Serikali kwaWatanzania Wanaoishi Nje ya Nchi Katika Kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM
Katika kutekeleza Ilani ya CCM Ibara 115 Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya awamu ya nne (4) inayoongozwa na Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete iliamua kuanzisha Idara maalum ya wa Uratibu wa Watanzania wanaoishi nje ya nchi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kadhalika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya awamu ya saba (7) katika kutekeleza Ilani hiyo ilianzisha Idara maalum ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Wazanzibar wanaoishi nje ya nchi.
Nafasi ya Watanzania Wanaoishi Nje Katika Mchakato wa Katiba
Kwa Watanzania na hasa Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi kwao mchakato wa Katiba unagusa maslahi yao katika maeneo mengi hususan suala la muuondo wa muungano na uraia wa nchi mbili. Serikali ya inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi katika kutambua umuhimu wa Watanzania wanaoishi nje ya nchi na kutekeleza ilani yake katika mchakato wa katiba mpya inapendekeza uwepo umuhimu wa kuwa na Uraia wa nchi mbili kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi (Dual Citizenship) pia Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi NEC ilipendekeza na kutilia mkazo uwepo wa raia wa nchi mbili. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika mchakato wa uteuzi wa wabunge wa Bunge la Katiba mpya alimteua mjumbe mmoja kutoka Marekani kuwakilisha Watanzania wanaoishi nje ya nchi. Aidha, Chama cha Mapinduzi kinaendelea kuchukua juhudi kuwaelemisha wananchi kupitia ziara na mikutano ya ndani na hadhara kuhusu maamuzi ya CCM ya kuendelea na mfumo wa Serikali mbili zilizoboreshwa na upotoshwaji unaofanya vyama vya upinza baada ya kususia vikao vya Bunge.
Wapinzani na Watanzania Wanaoishi Nje ya Nchi
Wapinzani wamekua mstari wa mbele kuwafata na kuwapa taarifa zisizokuwa za kweli Watanzania wanaoishi nje ya nchi hali ya kuwa CCM ndio chama pekee kinachotambua umuhimu wao na kudhamini michango yao hadi kupelekea Ilani ya Chama Cha Mapinduzi Ibara ya 115 kutamka kuwaekea mazingira bora na maslahi mazuri ili waendelee kuchangia maendeleo ya Tanzania.
Hoja naMadhumuni ya Ziara
Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM imeamua kwa dhati kuwafuata wana CCM na Watanzania hususan Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi kwa lengo la kwenda kuwaeleza utekelezaji wa Ilani na mikakati ya CCM kwa raia wake wanaoishi nje ya nchi (Diaspora), ikiwemo ufafanuzi kuhusu fursa mbalimbali za kuwekeza zinazopatikana nchini, kuwafanulia kuhusu mchakato wa Katiba tokea ulipoanza, ulipofikia na unapoelekea, kupokea maoni yao juu ya masuala mbali ambayo yanawagusa hasa suala la uraia wa nchi mbili na muuondo wa muungano na kuimarisha mahusiano kati ya Idara na wanachama, taasisi mbali mbali katika nchi hizo na kadharika.
Mikakati ya CCM
- Kuwapatia Uraia wa nchi mbili raia wote wa Tanzania wanaoishi nje ya nchi.
- Kuwaekea Sera bora rafiki ili waweze kuwekeza na kuchangia maendeleo ya Tanzania.
- Kubadilisha Sheria zote zinazowafanya kuwa wageni hali ya kuwa ni wazawa wa Tanzania.
Hitimisho
Kutokana na kuwa na wimbi kubwa la watanzania wanaoishi nje nchi CCM inakila sababu ya kujiimarisha ndani na nje ya nchi kwani wapinzani wamekuwa wakijilabu, hali ya kuwa CCM ndio chama Tawala na ndio chama pekee kwenye Ilani yake kinatambua umuhimu na mchango wa Watanzania walioko nje ya nchi na ilani kutamka kuwaekea mazingira bora pamoja na kubadilisha Sheria zinazowatambua kama ni Watanzania na si wageni. Vyama rafiki wa CCM kama ANC na FRELIMO vilitumia utaratibu wa kujiimarisha na kufungua matawi mengi ya vyama hivyo nje ya nchi na vinaonesha kufanikiwa na kupiga hatua sana. Aidha, kutokana na historia ya Zanzibar na utafaiti wa changamotoza kisiasa kati ya Watanzania wenye asili ya Bara na Zanzibar kuna haja ya kuandaa mkakati wa kipekee kupitia Idara hii utakawezesha kuongezea juhudi mbali mbali ambazo zimeshawahi kufanywa na Chama katika kuimarisha CCM nje ya nchi. Kwa hoja hizo Idara ya Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa inakila sababu na niwakati muwafaka wa kufanya ziara hizo za nje ya nchi.
BAJETI YA ZIARA2100
Ticket kwa watu 2 Zanzibar kwenda Dar es Salaam, kwenda UK, USA, CANADA na kurudi Tanzania itagharimu kiasi cha Dola za Kimarekani $3750 kwa kila mtu. Jumla gharama za ticket ni $7,500. Jumla ya gharama za kujikimu watu wawili kwa siku 9 ni $4,620 [UK (420x3) + Canada (350x3) + USA (350x3)] x 2. Jumla Kuu ni $ 12,120, kama inavyoneshwa katika mchanganuo ufuatao:
Mchanganuo na Ratiba yaSafari
No comments:
Post a Comment