Na Mwl Anthony Thomas Gella
AWALI ya yote naomba (nidiclear interest) Mimini muumini wa Rasimu ya pili ya Katiba na ni muuminiwa Katiba mpya, pia ni mshauri wa kujitegemea wa RaisJakaya Mrisho Kikwete katika suala la mchakato wakupata Katiba inayotokana na wananchi (Katiba ya 2014).
Hili la kuwa mshauri wa kujitegemea linajidhihirishapale nilipoandika waraka wenye kichwa cha habari “RaisKikwete linda zama zako” kwenye kichwa cha habarikidogo “kila zama zina mtu wake”
Na hii ni baada ya yeye mwenyewe Rais Kikwetekuamua kuanzisha mchakato wa watanzania kupataKatiba yao wenyewe, nasema yeye mwenyewe kwasababu suala la kuandika Katiba mpya halikuwa katika ilani ya chama chake 2010. Suala la Katiba mpya si tu halikuwepo katika ilani ya chama chake bali pia wasaidizi wake ndani na nje ya chama kwa maana ya mawaziri walishatamka wazi kuwa katiba iliyopo hainamatatizo inawafaa watanzania. Mawaziri hao nialiyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Selina Kombani, Mathias Chikawe na hata Mwanasheria wetu Mkuu wasasa Fredrick Werema aliungana na mawaziri wake.
Rais Kikwete bila kushauriana na wasaidizi wakendani ya chama na hata ndani ya Serikali aliamua yeyemwenyewe tarehe 31.12.2012 kuwatangazia Taifa katika salaamu za mwaka mpya kuwa ameamua kuwatengenezea watanzania Katiba yao na kufuatiwa na kuunda tume yamabadiliko ya Katiba, chini ya Mwenyekiti wake jaji mstaafu Joseph Sinde Warioba. Huo ndio msingi wamimi kusema “Rais Kikwete hatakiwi kulaumiwa kwaasilimia nyingi” kwa kuwa alifanya vile kama mtanzaniana kama Rais mwenye mamlaka. “Urais wangu haunaubia na mtu” (Dr. Jakaya M. Kikwete).
“Kama kuna wakati Rais Kikwete alitumia falsafa yake vizuri ya “akili za kupewa changanya za kwako” niwakati wa kutoa salaamu za mwaka mpya 31.12.2012alipolihutubia Taifa na kulitangazia Taifa kuwa ameamua watanzania waandike katiba yao wenyewe”.
Lawama kwa Rais Jakaya Kikwete zilikuja pale alipokuwa akilihutubia bunge maalumu la Katiba wakatiwa uzinduzi wa “bunge maalumu la katiba” hapo akili za kupewa au kusikia hakuchanganya na za kwake bali alijikuta analihutubia bunge hilo kama anahutubia NECya CCM. Badala ya kukaa katikati, aliamua kuwa mwanaccm kamili, ndipo alipofungua mlango walawama.
Hata baada ya uamuzi huo mzuri wa Rais Kikwete kuwaletea wananchi Katiba yao, kuna wanachama wachama cha mapinduzi walianza kumlaumu kwa hatua yake hiyo, kwa mfano mwanasiasa mkongwe na kadawa CCM Kingunge Ngombale Mwiru aliibuka nakumlaumu Rais Kikwete hadharani kuwa kitendo chakutangazia Taifa kuanzisha mchakato wa uundwaji wa Katiba mpya ni kushabikia hoja ya wapinzani (CHADEMA) ambao walidai kama watapewa ridhaa nawananchi kutawala, ndani ya siku 100 wataanzishamchakato wa kupata katiba mpya.
Mimi kwa kuona Mhe Rais Kikwete hawezi kumji bukada mwenzake Kingunge Ngombale Mwiru na baadaya kuguswa na lawama zile kuwa hazikuwa sahihi. Nilimjibia Rais Kikwete kwa kuandika makala katika gazeti hili la Tanzania Daima toleo Na………. la tarehe 4 Septemba 2013 yenye kichwa cha habari “Kingunge amepitwa na wakati” kwani Rais alifanya vile kama mtanzania mwenye mamlaka ya urais siyo kama mwenyekiti wa CCM.
Baada ya hatua zote hizo mimi nilijipendekeza kuwa, mshauri wa kujitegemea wa Rais Kikwete na hii nibaada ya kuona wasaidizi wake ndani ya chama na ndaniya Serikali wakitoa matamko ya kumkatisha tamaa, niliandika waraka huo wenye kichwa cha habari “Rais Kikwete Linda Zama Zako” wenye kichwa kidogo kisemacho “KILA zama zina mtu wake”.
Katika waraka huo nilionyesha kila mtangulizi wake alivyo ingia katika historia. Baba wa Taifa, alituletea uhuru wa bendeara na kuwaunganisha watanzania kuwawa moja na kuziunganisha Tanganyika na Zanzibar nakuzaa Tanzania tunayojivunia.
Rais Ali Hassan Mwinyi aliacha historia kwa kuruhusu mfumo wa soko huria uliopachikwa jina la“ruksa”. Na Rais Benjamin Mkapa yeye ana historia ya kuinua uchumi, kuthibiti mfumuko wa bei na kuifanya fedha kuwa na thamani kubwa.
Nilimshauri yeye alinde zama zake kwani “ana dalili za kuingia katika historia maalumu ya kuwaletea watanzania uhuru wa kumiliki uchumi wao kupitia kuandika katiba yao wao wenyewe, kupitia kutoa maoni ya jinsi gani wamiliki Rasilimali zao na jinsi gani watawaliwe na viongozi wao tofauti na Katiba iliyopo”.
Aidha nilimshauri ili aingie katika historia hiyo asilitumie/asilibadilishe bunge hili la kutunga sheria nakusimamia Serikali kuwa bunge maalumu la katiba, kwakuwa bunge hili limekaa kiitikadi zaidi. Nawafahamuhawa vizuri zaidi, kama walishindwa kutunga sheria tu yakuweka mchakato wa bunge lenyewe hadi wenginewakatoka nje na kufikishana kwako, hatutakuwa na imaninao tena kuwapa Rasimu yenye ibara zaidi ya 227, lakinikwa bahati mbaya ushauri wangu hakuuchukua kwa kuwanilikuwa mshauri wa kujitegemea pamoja na nakala yaushauri huo kuupeleka Ikulu na kupokelewa tarehe25/10/2013 saa 10:30 asubuhi.
Kinachotokea sasa pale bungeni ndichoniichomtahadharisha, kulitumia bunge la kutunga sheriana kuisimamia Serikali kuwa wale ndugu wamekaakiitikadi zaidi kuliko uzalendo na hili lilijionyesha waziwakati wa kupata wenyeviti wa zile kamati 12 na hatakwenye uteuzi uliofanywa na Mwenyekiti, naulijionyesha wazi zaidi kuanza kuchakachua/kutenguakanuni hata bado hazijatumika.
Kama Rais angelifuata ushauri wangu wa kufutasheria iliyowapeleka bungeni, wabunge wa Jamhuri yamuungano na wale wa Zanzibar na badala yake sheriaiseme “Wabunge wa bunge maalumu la Katibawatachaguliwa katika Wilaya zao bila kudhaminiwana chama chochote cha siasa”. Malalamiko yaliyotokeakuwa wenyeviti wote wamekuwa wa chama kimoja(CCM) na Kamati ya uongozi kuwa na wajumbe wachama kimoja (CCM) yasingekuwepo. Hata Mwenyekitiwa bunge maalumu la Katiba Samwel Sitta amesemabunge maalumu limetekwa na wanasiasa baada ya yeyekuonekana ameshindwa kuliongoza.
Kile ambacho nilimshauri Rais Kikwete kwenyewaraka wangu, waraka ambao nilimpelekea Ikulu25/10/2013 miezi minne iliyopita kuwa asilitumie bungehili la kutunga sheria na kusimamia Serikali kama bungemaalumu la Katiba kwa kuwa limekaa kisiasa zaidi kulikokizalendo, ndicho kinachotokea sasa pale Dodoma. Walewabunge wa CCM na wapinzani hawaaminiani,wanaviziana kuanzia kwenye kanuni watakwenda hadikwenye kujadili Rasimu na kusababisha tusipate Katibatuitakayo hapo ndipo Rais atapata lawama kwa kulibadilibunge la kutunga sheria kuwa bunge maalumu la Katiba.
Nikiigeukia hotuba aliyoitoa Rais Kikwete, wakatiwa kuzindua Bunge maalumu la Katiba, Rais Kikwetealitakiwa azungumze kama mtu wa kati kwa kuwashauripande zote zinazovutana katika mambo mbalimbali iliwapate Katiba ya wananchi, Rais Kikwete alifeli kutumiafalsafa yake yeye mwenyewe “akili za kupewachanganya na zako” badala yake alitumia akili zakupewa na wasaidizi wake na kuonekana kamaMwenyekiti wa CCM na siyo kama Rais wa nchi.
“Mhe Rais Jakaya Kikwete bado una nafasi yakulinda zama zako”
Mwl Anthony Gella
E-mail: agella72@yahoo.com
Simu Na. 0656 907751
No comments:
Post a Comment