Na Bryceson Mathias
‘Samaki Mkunje angali Mbichi’....
NIMEKEREKA na kufikia mahali pa kuichukia Tume ya Uchaguzi nchini (NEC) kupitia Viongozi wake, kwa kuwa wana Unafiki wa kila siku kuwa na kauli za kudai inavionya Vyama ya Siasa kwa Maneno bila kuchukua hatua za Vitendo.
Mwenyekiti wa Tume, Makamu na Msajili, kila chaguzi wanadai wanavionya vyama vya siasa kuwa, hawatavumilia tabia na vitendo vya wagombea wa vyama vya siasa kutoa lugha chafu za kashfa dhidi ya wagombea kipindi cha kampeni, lakini utekelezaji wake, katu hauonekani.
Mara kadhaa NEC mejigamba haitavumilia tabia zisizo za kiistarabu, zinazochochea vurugu, watu kudhalilishwa kwa lugha za kashfa, ila Kalenga na Chaguzi za Kata 29 tumeshuhudia Watu kutekwa, kujeruhiwa na hakuna hatua za NEC tulizoziona ila kuneemeka kwao.
Bila kuweka wazi hatua ilizochukua dhidi ya vitendo vilivyotokea Kalenga, Msajili Msaiizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza kwa mara nyingine Jumapili Machi 30th, mwaka huualivionya tena Vyama na Vikundi vyao Ulinzi kufanya Kampeni za Kistarabu Chalinze.
Nyahoza alijinadi katika mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Maasai Lungwe,Chalinze; kwamba Kampeni zinaendelea vizuri, ingawa kuna malalamiko kidogo juu ya uvunjwaji ama ukiukwaji wa sheria za uchaguzi na malalamiko hayo yapo kwenye vyombo husika yanafanyiwa kazi.
Tabia hii ya maneno matupu inanikera kwa sababu tume hiyo imekuwa si msaada kwa watanzania, na badala yake imekuwa msaada kwa watawala kinyume na muundo na kinavyotakiwa kufanya kazi kiuhalisia.
Kwa nini NEC siipendi na inanikera; Ni kwa sababu inawatumainisha wapiga kura kwa kuwapa haki isiyokuwepo, ambapo Viongozi na wananchi wanashikishwa haki hiyo kwa Mkono wa Kushoto, halafu haki hiyo hiyo inawanyang’anya kupitia Mkuno wa Kulia.
Muda mrefu kumekuwa na Malalamiko yanayohusishwa na kupigwa kwa Viongozi na kujeruhiwa, wafuasi wa vyama kwenda kufanya kampeni kwenye mikutano ya vyama vingine, kushushwa na kuchannwa kwa bendera pamoja na rushwa hasa za kununua shahada za kupigia kura.
Pia kumekuwa na vitendo vya lugha za kashfa na dhihaka zinazoendelea wakati wa za maeneo mbalimbali, lakini NEC na Ofisi ya Msajili, imekuwa ikiishia kulaani na kudai vya viepuke vitendo hivyo, lakini hatua hazichukuliwi.
Msajili na Ofisi yake kila siku amekuwa akivionya Vyama kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutoa taarifa kwa vyombo husika, lakini cha kusikitisha, Maovu ya wahusika ni Aibu.
Moja ya kazi za Msajili na NEC ni kufuatilia Malalamiko ya Uvunjifu wa Sheria ya Wadau na Vyama, ili kujua ukweli wake na kuchukua hatua stahiki, lakini tume ina Ubovu wa kutochukua hatua hizo.
.
NEC ina Ubovu; Ubovu ni uleule uliyomo kwenye Daftari Bovu la wapiga kura, na ili kuondoa hali hiyo, lazima Uchama wa Zidumu Fikra za Mwenyekiti na maagizo ya watawala ndani ya NEC, yang’olewe ndipo haki itaonekana.
Ni wakati muafaka NEC ifahamu, Watanzania wasio vipofu wa mawazo, Macho na masikio, wamechoshwa na Kauli za alinacha za NEC nchini, kutokana na sura yake kuonekana ni NEC ya Chama Tawala na Viongozi wake..
Samaki Mkunje angali Mbichi akikauka atavunjika. NEC imeshakauka kwa hoja na haki hivyo haiwezi kuchukua hatua zozote; Makanwa yake yamekamatwa.
No comments:
Post a Comment