Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Wednesday, February 12, 2014

Wanasiasa wakiwakosea watanzania, Wasiende kutubu Ulaya!

‘Ukimkosea Mkeo, Usitubu kwa Mchungaji au Shekhe, Patana naye kwanza’.

Na Bryceson Mathias

KATIKA siku za hivi karibuni, wanasiasa wamebuni mbinu za kujisafisha, ambapo pamoja na kuwakosea watanzania kiasi hata cha kumwaga damu zisizo na hatia, wamekuwa wakikimbilia nje kwenda kutubu kwa wachungaji au kuhiji wakiacha kutubu kwa waliowakosea. 

Ikitokea umemkosea Mwenzi wako, usikimbilie kwa Mchungaji au Shekhe kutubu na kuomba Msamaha kwa maana ya kuwa utamaliza ugomvi la hasha! Ujue Mchungaji au Shekhe, siyo uliowakosea, ila patana na mwenzi wako kwanza, ndipo muongozane ukatubu kwao.

Biblia Mathayo.18:15-19 inasema, “Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo. La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike. 

“Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.

“Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni. 

“Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni”.imesisitiza Biblia ambacho ni kitabu kitakatifu.

Mwanaume mmoja alifumaniwa na mkewe, wakagombana na mwenzie kimyakimya usiku mzima! Asubuhi mwanaume akadamka kwa Mchungaji akamweleza kisa na mkasa, akapewa toba! Lakini aliporudi nyumbani, ugomvi ulizidi ule wa usiku, tenasasa ukawa hadharani.

Kosa la mwanaume huyo lilikuwa kwenda kwa Mchungaji bila kwanza kupatana na waliyekosana naye (mkewe), ambapo baada ya hapo hata kama angekwenda kwa Mchungaji, hatimaye kurudi nyumbani, kusingekuwa na ugomvi tena.

Nataka wana siasa waelewi hivi, Mungu si kama Tetea wa kudanganywa na Jogoo kwamba, kwamba nitakununulia gauni la kumzuguka mwanzo wa kichwa huku akiburuza mbawa zake kuonesha urefu wa gauni lisiloshonwa kila siku.

Mungu anasema katika Mathayo 5:25  “Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani.

Galatia 6:7  anasema; Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.

Yohana 9.31  anasema, Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo”.

Mfano; Mtu anakimbiliaje kwa TB Joshua nchini Nigeria, kufanya toba, kuombewa au kupata kile kinachoaminika kuwa ni utakaso, wakati hujapatana na uliowakoseaTanzania? Huko ni kumbusu Kware aliyenaswa kwenye Mtego badala ya kuushukuru Mtego uliopinda siku zote na kumnasa.

Kwa kosa hilo, mshitaki wako atakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani. Kwa maana ya kwamba ukirudi dhambi zile ziko pale pale, ni sawa na kuoga halafu ukavaa nguo chafu.

Ni rai yangu wanasiasa watambua, kukimbilia makanisani au misikitini kuombewa, kufanya toba na kufanya Harambee, si kupata utakaso unaoaminika unaweza kuwasaidia katika harakati zao za kisiasa bila kupatana na washitaki au wadeni wao, kunaweza kuwa Laana kubwa!
 Ieleweke, Damu ya watanzania inayomwagika kila siku kwenye chaguzi ndogo na kubwa nchini au migogoro, zitatakwa kwa viongozi wanaohusika na uvunjifu wa amani, hawataachwa salama na mkono wa Mungu.

Biblia katika Ezekieli 33:8-9 inasema, “Nimwambiapo mtu mbaya, Ewe mtu mbaya, hakika utakufa, nawe husemi neno la kumwonya mtu huyo, aiache njia yake, mtu mbaya huyo atakufa katika uovu wake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.

“Walakini ukimwonya mtu mbaya kwa sababu ya njia yake, kusudi aiache; wala yeye asiiache; atakufa huyo katika uovu wake, lakini wewe umejiokoa roho yako”.

Wanasiasa watambue, hata tuwe na Katiba Mpya, lakini kwa malengo mabaya ya kisiasa, yanayofanywa na baadhi yao kila siku iendayo kwa Mungu kwa hila, yanaandikwa kwenye Daftari la Mungu na Malaika kupitia Pumzi kama Peni. Mithali. 20:27.

Unapoagiza jambo Baya au Zuri lifanyike, kinachotumika ni Pumzi, hivyo pumzi iliyotumika kuua, kusema uongo, kutesa, kuiba, rushwa, kudhulumu, kufanya ufisadi, kufanya usaliti na kila jambo linalofanana na hayo; Mungu anaona pumzi yake ikitumika; atahoji inatumika kwa haki?!

No comments: