Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Wednesday, February 12, 2014

Wananchi watoa up dates za Jimbo la Kalenga kwa Chadema’!

Na Bryson Nyeregete
WAKATI Chadema kimepanga kumtangaza mgombea wa kiti cha Jimbo la Kalenga wakati wowote baada ya Kamati Kuu ya chama hicho kuketi mwishoni mwa wiki hii kwa ajili ya kuteua jina la mgombea, Wananchi waliohojiwa wametoa ‘up dates hizi’ kwa Chadema ili zifanyiwe kazi.

Wananchi hao wamedai wanakiomba Chadema, pamoja na viongozi wote kutumika kulishambulia Jimbo la Kalenga, lakini watuitumie Timu iliyohusika katika Mchakato wa Kampeni za Arumeru, Arusha, ambapo Mbunge Joshua Nassari aliibuka Mshindi.

Wamesema, katika chaguzi za Kata 27 zilizopita, wamebaini kumekuwa na vitisho vya kauli ambavyo vilitangazwa na viongozi wa CCM, akiwamo, Nape Nnauye, lakini wamebaini maeneo kadhaa kulikuwa na nguvu ndogo ya kulinda kura na udanganyifu; hivyo uwajibikaji uongezwe!

Kwa sasa Chadema kinakusanya fomu za waliojitokeza kugombea jimbo hilo… ambapo hadi wakati huu, kinaendelea na zoezi hilo, ambapo mwamuzi wa mwisho ni kamati kuu itakayoketi mwisho wa mwezi huu kwa ajili ya uteuzi wa jina hilo.

No comments: