Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Friday, January 31, 2014

Dk. Slaa ataja mwarobaini wa migogoro ya ardhi nchini


Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk. Willibrod Slaa, amesema migogoro ya wakulima na wafugani haitaisha ikiwa hawatatengewa maeneo yao maalumu. Aliyasema hayo, wakati akihutubia mamia ya wakazi wa mji mdogo wa Mheza uliopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga. Alisema wakulima na wafugaji mpaka sasa wanaendelea kugombana na hawana amani katika nchi yao kwa sababu ya migogoro inayoendelea kati yao. Alisema kumaliza migogoro ya pande hizo mbili na kuepuka hatari inayoweza kutokea, ni vyema wakatengewa maeneo rasmi kwa ajili ya shughuli zao. Kadhalika, alisema Watanzania wanahitaji kuunganisha nguvu zao ili wapate haki yao ambayo itawaletea amani ya kudumu. “Pasipo na haki hakuna amani, wakulima na wafugaji wanaendelea kugombana kwa sababu ya kila mmoja anatafuta haki, mwingine anatafuta haki yake ya kulima na mwingine haki ya kufuga na ndiyo maana wanagombana,” alisema na kuongeza:

“Hatutaki makundi haya yaendelee kugombana, tunataka migogoro yao itatuliwe  kwa kila pande kupatiwa eneo lake, hii italeta amani kati yao.” Dk. Slaa alisema amani haipatikani kwa mahubiri tu bali katika kutenda haki kwa kila mmoja anayestahili kuipata. Alisema kati ya mikoa ambayo ina wafugaji na wakulima wengi ni mkoa wa Shinyanga, hivyo unapaswa kuangaliwa kwa jicho la upendeleo kwa kuhakikisha unatengewa maeneo ya kutosha kwa wakulima na wafugaji


Zaya E. Ippmedia/Nipashe

No comments: