![]() |
Ben Saanane |
Kuna Kelele nyingi sana juu ya
viongozi kusafiri nje ya nchi.Kuna baadhi ya wana-CCM wanajaribu kutumia Safari
ya Dr.Slaa nje ya nchi kuhalalisha safari za Kikwete alizofanya nje ya nchi.
Rais Kikwete amesafiri mara 357
tangu aingie Madarakani kwa kipindi cha miaka 7 na miezi kadhaa akitumia Kodi
za watanzania ambao wanaambiwa kwamba ni lazima wachangie kodi ya laini za simu
hata kama wapo kijijini na kutumia laini hizo kuwabip watoto wao walioko mjini
bila kazi maalumu.Kodi hizo ni sehemu ya kugharamia safari hizi za Rais kama
nitakavyoonyesha pichani hapo chini.Katika siku 357 alizosafiri, zimepungua
siku 8 tu akamilishe mwaka wenye siku 365. Hapa tumeongelea safari ya siku moja
tu,kuna nyingine amekaa nje zaidi ya wiki na nyingine wiki 2 kama hii
aliyoifanya juzi.Safari nyingine sio Muhimu hata kidogo.Kuna nyingine zinamhusu
waziri wa Mambo ya Nje,nyingine zinawahusu Mawaziri wa Utalii na hata
Wakurugenzi wa Idara.Delegation of power(Kukasimisha madaraka) haipo katika
Utendaji wake.Hata kama Rais hana Management skills,washauri wake walitakiwa
kumshauri na kumwambia ukweli kuhusu hili.
Sasa hivi dunia ni kama kijiji,ni
lazima tutumie fursa ya teknolojia.Sio Lazima kwa Rais kusafiri na kuwepo
kwenye mkutano physically.Baadhi ya Mikutano hufanyika kupitia Mitandao.Balozi
zetu nje zinaweza kuwa empowered na kuiwakilisha serikali kwenye mikutano
mingine ya uwekezaji.Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe mara kadhaa amekua
akiongea kama vile ni mtu anayeelewa sana dhana ya Economic Diplomacy.Sijui ni
kwanini hataki kumshauri Rais Kikwete ambaye nina uhakika hana taaluma ya
Diplomasia na Uhusiano wa kimataifa au hata taaluma yenye uhusiano na fani hiyo
ingawa alijitutumua kisiasa alipokua waziri wa Mambo ya nje.Pamoja na kuwa na
shahada ya Uchumi ya miaka hiyo ya 1970,sidhani kama Rais wetu( kama ilivyo
kawaida ya Waafrika wengi) alifanya jitihada za kuendelea kujisomea nadharia
nyingine au kujiendeleza kitaaluma(hata kwa kozi fupi) kulingana na mabadiliko
ya Dunia ukizingatia kuwa alijiandaa kwa Miaka 10 kuwa Rais wa nchi(Kama
alivyokiri mwenyewe).Diplomasia ya Uchumi alitakiwa aielewe.Sio busara
kujiandaa kwa kujikusanyia mashabiki bila wewe kujiandaa kitaaluma kulingana na
mahitaji ya muda.Ni uzembe na usalaiti.
Rais wa Zamani wa Nigeria Olusegun
Obasanjo ndiye Mtawala aliyeweka Rekodi ya kusafiri mara nyingi zaidi.Viongozi
wa Afrika wakisafiri mara nyingi hutumia gharama kubwa na misafara
mikubwa.Matumizi mabaya ya fedha. Tanzania sasa inabidi kuwe na tume ya
kudhibiti Ziara za Rais maana kama ndani ya Miaka Saba na miezi kadhaa Rais
Kikwete amekaa nchini kwa miaka 6 tu sasa tunaelekea wapi?
Rais amesafiri nje ya nchi kwa
wastani wa safari 45 kwa mwaka 1.Ni wastani wa safari 4 kwa Mwezi 1.Ni wastani
wa safari 1 Kila wiki. Katika siku 5 za kufanya kazi kiofisi(Sheria zetu za
kazi ziangaliwe upya),Rais anasafiri nje ya nchi siku 1.Yaani kuanzia Jumatatu
hadi ijumaa,siku 1 Rais yupo safarini nje ya nchi kwa siku moja.Hapa
hatujajumuisha idadi ya siku anazokaa humo
Waziri wa Mambo ya nje angesafiri
hivyo tungemuelewa lakini kwa sababu za msingi.Aliyekua waziri wa Mambo ya nje
wa Marekani(Taifa lenye Nguvu duniani za kiuchumi na Kijeshi) Bi.Hillary Rodham
Clinton alikua muumini wa Falsafa ya Msanii wa Brooklyn,Woody Allen kuwa
asilimia 80 ya mafanikio ya makubaliano au kikao chochote muhimu ni Uwepo wako.
She reinforced the power of being there -- in a place, in a context, in
a moment. Hillary aliweka rekodi ya kusafiri masaa 2,084.21 sawa na wastani wa
siku 86.83 na jumla alisafiri siku 401.Huyo ni mtu aliyekua waziri wa mambo ya
nje wa Taifa lenye ushawishi duniani kwa maslahi ya Taifa lake huku Rais
akisafiri mara Chache.Alipokuja Tanzania Rais aliacha kazi zote na kuvuruga
itifaki,alienda Kumpokea badala ya Waziri wa mambo ya nje kuchukua nafasi
yake.Delegation of power hapa sijui ilikua in a reverse order ama ni nini?!
Mwalimu Nyerere katika Miaka 24 ya
utawala wake alisafiri mara 60+ lakini JK kwa mika isiyofika 8 amesafiri
karibia mara 360. Tunaambiwa(Kwa kufuata utamaduni wake ule wa kuambiwa) kuwa
safari moja ni zaidi ya Sh.300,000,000(milioni 300) na pia tukifanya kuwa kila
safari moja kwa kiwango cha chini anakaa siku 3 maana yake ni (357 X 3.12) sawa
na siku 1071 ambayo ni sawasawa na miaka 2 na miezi 9 ,wiki 3,siku 4, masaa 4
na dakika 3, na sekunde 30 nukta 3.Huyu ndiyo Rais wa nchi ambayo ni miongoni
mwa nchi Maskini duniani ambaye zaidi ya asilimia 50 ya Raia wake wanaishi
chini ya dola moja ya Marekani kwa siku yaani zaidi ya nusu ya watanzania
milioni 45 ambayo ni sawa na watu milioni 22.5(22,500,000) hawawezi kumudu
matumizi ya Shilingi 16,00/ kuanzia saa 12 alfajiri hadi saa 12 alfajiri ya
siku inayofuata.Rais
Hajui ni kwani hali hii imekua
hivi,hata yeye anashangaa.Hata hivyo ili kufidia nakisi ya bajeti(deficit) ya
shilingi bilioni 264,inabidi Raia hawa hawa watozwe kodi ya laini za Simu kwa
mwezi.Safari za Rais hadi muda huu kwa wastani niliotaja umegharimu
sh.107100000000(Zaidi ya Bilioni 107) ambazo ni karibia Nusu ya kodi ya laini
itakayotozwa Tanzania nzima kutoka kwa wamiliki milioni 22 wa laini za simu
ambao takwimu zinaonyesha milioni 8 kati yao hawana uwezo wa kutumia shilingi
1000 kwenye simu zao kwa siku.Wanatumia kwa Sms na kubip tu.Maskini
wanagharamia safari hizi ambazo mara nyingi Rais amekua akijitetea za kutafuta
wawekezaji zinaishia kuvuta hata wawekezaji ambao takwimu zinaonyesha kwa
mujibu wa utafiti uliofanywa na Interfaith Standing
Committee on Economic Justice and the Integrity of Creation mwaka jana
uligundua kuwa kwa wastani Tanzania hupoteza dollar billion moja (takriban shs
trilioni 1.8) kila mwaka kutokana na ukwepaji kodi, uhamishaji harama wa fedha
na misamaha ya kodi.
Je ziara zote za Rais
Kikwete zina manufaa na tija kwa taifa letu?Katibu Mkuu wa CHADEMA na aliyekua
mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2010 kwa tiketi ya
CHADEMA Dr.Wilbroad Slaa yupo nje ya nchi.Amesafiri mara chache na kwa kazi
maalumu za kiofisi.
No comments:
Post a Comment