Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Dr. Wilbrod Slaa, katibu mkuu
wa Chadema amefanya mahojiano na radio ya Indianapolis ambayo ndiyo moja ya radio
kubwa nchini marekani akisikilizwa na watu zaidi ya millioni 9 huku wengine
wakishiriki kwenye mjadala kupitia mitandao ya jamii na simu moja kwa moja.
Kwa asilimia kubwa, wengi wamemkubali na kumuona kama mkombozi,
siyo tu wa Tanzania, bali wa bara la Afrika kutokana na jinsi alivyojielezea na
pia kuzungumzia mada mbalimbali hasa mikakati yake na chama chake Chadema
kumuokoa mtanzania kutokana na ukoloni mamboleo ya CCM. Dr. Slaa amezungumzia
kuhusu elimu, kilimo, afya, uwekezaji na fursa nchi zilizopo Tanzania.
Baadae mchana, Dr. Slaa atahojiwa na radio ya jijini Washington
DC. Stay tuned...
![]() |
Dr. Slaa akiongozwa |
![]() |
Dr. Slaa akijadiliana na Minority leader wa bunge la Indiana |
![]() |
Dr. Slaa akifurahia jambop ndani ya studio |
Mchana huu atakuwa hapa;...
Dr. Slaa interview na Washington, D.C., U. S. A. Pacifica station WPFW 89.3 FM., Jumatano, Oct 9, 2013
Dr. Wilbroad Slaa amealikwa kwa mahojiano na WPFW Radio ya Washington, D.C., U.S.A. siku ya jumatano October 9, 2013. Saa saba mchana kwa saa za Amerika ya mashariki (1pm U.S Eastern time)/ Saa mbili usiku saa za Afrika mashariki (8pm East Africa time).
Kumefanyika jitihada za kuushirikisha ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kushiriki mahojiano haya bila kuwa na mafanikio. Bado jitihada za kuushirikisha ubalozi zinafanyika mpaka hivi sasa.
Baadhi ya mambo yatakayo jadiliwa ni hali ya siasa Tanzania, hali ya kijamii, hali ya kiuchumi, amani na usalama wa Tanzania na mengineo.
Bofya hapa kusikiliza WPFW radio live WPFW Radio
No comments:
Post a Comment