![]() |
Wenje |
![]() |
Chenge |
“Sera ya Mkapa ya kubinafsisha viwanda imesababisha wananchi wengi kukosa ajira na nchi kuyumba kiuchumi. Maana viwanda vingi vilivyochukuliwa wa wawekezaji vimekufa na kubaki magodauni ya kutunzia mali za wawekezaji hao. “Kutokana na ukweli huo, ndiyo maana vijana wengi sana kwa sasa hivi wametumbukia kwenye biashara ya umachinga na kuendesha bodaboda. Na CHADEMA tunaomba mtupe nchi mwaka 2015 ili tuwakomboe na lindi la umaskini uliopo sasa,” alisema. Kuhusu fedha za rada, Wenje alimtuhumu pia aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM), kwa madai kwamba ndiye aliyeliingizia taifa hasara kubwa kutokana na manunuzi ya kifisadi juu ya chombo hicho. Alisema kwamba manunuzi hayo ya kifisadi yalishtukiwa na Serikali ya Uingereza, hivyo kuamuru fedha zilizozidi zirudishwe nchini kwa ajili ya kusaidia miradi ya maendeleo, lakini fedha hizo hazijulikani zilipo kwa sasa.
“Chenge na serikali ya CCM walifanya manunuzi ya kifisadi kuhusu rada. Yaani manunuzi hayo yaliishtua hadi Serikali ya Uingereza na kuhoji kwa nini Tanzania nchi maskini inunue rada kwa bei kubwa hivyo?”alihoji. Aidha, aliwaomba wananchi wa Nyamagana kujiandaa kuiangusha CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani, pamoja na uchaguzi mkuu 2015, kwani imeshindwa kuwaletea maendeleo wananchi wake. Hata hivyo, mbunge huyo Wenje aliwaahidi wananchi wa Kishili, Kata ya Igoma kushughulikia suala la umeme ili waweze kupata nishati hiyo kwa ajili ya maendeleo yao.
Source: Suma S. (Oct. 2013).Wenje awachokonoa Mkapa, Chenge. Retrieved from Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment