Akiendelea na ziara yake
nchini Marekani ya kujifunza inayoItwa “Vision Tanzania”. inayolenga kutafuta
ufumbuzi wa tatizo sugu la, Katibu mkuu wa Chadema Dr. wilibrod Slaa, jana
ametembelea maeneo mbali mbali yanayoendana na Nishati. Moja ya maeneo hayo ni
eneo kubwa la kutengeneza umeme wa upepo “wind firm” huko Indiana,
linalotengeneza zaidi ya MW 550, pamoja na solar farm linatogengeneza kiasi cha
MW 20.
Vile vile Dr. Slaa ametembelea Chuo kikuu cha utafiti cha Purdue,
kitivo cha Engineering ambako alijionea ubunifu na utafiti wa hali ya juu
unaofanywa na wanafunzi pamoja na walimu wa chuo hicho. Kwa masikitiko makubwa,
Dr. Slaa amesema kwamba, CHADEMA haina jinsi zaidi ya kutafuta mbinu mpya ya
kuweza kuwaokoa watanzania kutoka kwenye shimo la umasikini na minyonyororo ya
CCM.
 |
Kiongozi mwenye machungu. Lazima ukombozi upatikane |
Rais Kikwete mwenyewe
ameshakiri wazi kwamba hajui ni kwa nini watanzania ni masikini. Kwa hiyo kama
hajui kwa nini Watanzania ni masikini, basi yeye na CCM, ni bora wakawarudishia
watanzania nchi yao. Hii ndio sababu kubwa CHADEMA inahangaika kutafuta
ufumbunzi
Tatizo la umeme ni mradi wa mafisadi ndani ya CCM. Tanesco
linafirisika kutokana na mapato yake kulipia mafuta mazito na makampuni kama
Symbion.
Ziara hiyo ya Dr. Slaa ambayo imeratibiwa na Umoja wa vyuo vikuu
vikubwa marekani, imelenga zaidi kutafuta ufumbuzi wa matatizo sugu
yanayomkabili mtanzania.
Dr. Slaa na CHADEMA
wamedhamiria kuliokoa Tanzania kushirikiana na mataifa pamoja na mashirika
ambayo yatafanya biashara ya usawa na Tanzania. Hatutaki rasilimali zetu
kupelekwa kuendelea mataifa mengine wakati tunarudishiwa bidhaa
bandia.
Inafika muda binadamu anayenyanyaswa anasema basi. Watanzania
wamechoka !
 |
Vision Tanzania in the Horizon |
 |
Dr. Slaa waadhiri wa Purdue University pamoja na mwanafunzi mtafiti |
 |
mwanafunzi mtafiti akimuelezea dr. slaa jinsi micro grid yake inavyofanya kazi |
 |
Shamba la Mega Watts 20 |
No comments:
Post a Comment