Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia
na Maendeleo , CHADEMA, Dr. Wilbroad
Slaa leo Jumapili 13 Oktoba amesafiri
kurudi Tanzania baada ya Ziara yake iliyomchukua wiki tatu nchini Marekani. Dr Wilbroad aliwasili nchini Marekani tarehe 21 Septemba, 2013, akiambatana na Mkewe
mama Josephine Mushumbuzi na kupokelewa na Uongozi wa CHADEMA DMV. Tarehe 22 Septemba, 2013, Dr. Slaa alifanya
mkutano uliojumuisha wanajumuia ya Watanzania waishio katika Majimbo ya
Washington, Maryland na Virginia.
Katika ziara yake Dr. Slaa alitembelea
majimbo ya North Carolina na Alabama ambako alitembelea Vyuo Vikuu na Taasisi
mbalimbali na kujifunza Shuguli nyingi za Maendeleo katika Sekta mbalimbali
ikiwemo Kilimo, Afya, Nishati na Uchumi.
Akizungumza akiwa uwanja wa Ndege wa
Dulles Virginia kilometer chache kutoka Wshington, D.C., Dr. Slaa alisema
alichojifunza akiwa Marekani anatarajia kupeleka maarifa hayo Tanzania ili
yaweze kumkomboa Mtanzania kutoka katika Umaskini. Moja katika mambo ambayo
amejifunza ni namna ya kutumia nishati ya Jua kuzalisha umeme hasa kwa wakazi
wa Vijijini.
Dr Slaa amekamilisha ziara yake ya wiki
tatu nchini Marekani iliyopewa jina la “Vision
Tanzania” baada ya kualikwa na Umoja wa Vyuo vikuu nchini Marekani.
No comments:
Post a Comment