Taarifa zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii pamoja na baadhi
ya magezeti (Uhuru, Jambo leo, na Majira). Kuhusu kuhama kwa viongozi na
wanachama wa chadema na hivyo kupelekea kufungwa kwa ofisi ya Chadema wilaya ya
Handeni sio za kweli bali za kupikwa.
Mtakumbuka kuwa imekuwa kawaida ya ccm kusema na kuzusha uongo
ili kuendelea kuhadaa watu kwa manufaa ya siasa nyepesi ili kukwepa kujibu au
kutatua mambo mazito yanayo kabili jamii na taifa kwa ujumla.
UKWELI NI UPI
1. Shabani Ngido aliyetajwa kama katibu hakuwa katibu wala
mwanachama wa Chadema, katibu halali wa Chadema wa wilaya ya Handeni anaitwa
Ramia Ibrahimu Kisalazo anaishi Mkata umbali wa zaidi ya kilometa 20 kutoka
Handeni mjini. Huyo Shabani Ngido alikuwa mwanachama wa ADC hakuwahi kuwa mwanachama
wa Chadema.
2. Ni kweli mwenyekiti wa wilaya Bwana Lucas Elisa Selemani
amehamia ccm kwa sababu anazojijua yeye moja kubwa ikiwa ni pamoja na kutishiwa
kuchomewa tena nyumba. Alisha chomewa nyumba mara ya kwanza na wafuasi wa CCM.
3. Idadi ya wanachama zaidi ya 300 iliyo tolewa kuwa wamehama
Chadema sio ya kweli na imejaa takwimu za uwongo. Wanachama walio kihama
Chadema na kuhamia ccm haizidi 10, miongoni mwa hao kuna aliyetajwa kuwa
alikuwa mwenyekiti wa Kabuku, hakuwa mwenyekiti bali mwanachama wa kawaida.
4. Baadhi ya wanachama wa ccm walipewa kadi bandia ili watakapo
zirudisha ijenge taswira kuwa wanahandeni wameanza kuikataa Chadema, hili
limefanyika kwenye ziara nyingi za mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi ya ccm.
Mfano ukiwa wilaya ya Hai ambako kadi na walioitwa wanachama wa Chadema zaidi
300 walitajwa kuwa wamerudisha kadi na kurejea ccm wakati ilikuwa ni uwongo.
5. Ccm walidiriki kununua bendera za chadema kati ya shilingi
20000 na 30000 ili zisipepe kwenye maeneo ambayo Bulembo alikuwa anapita au
kwenda kufanya mikutano na kushindwa kujali na kutatua shida ya maji inayo
ikumbuka wilaya ya Handeni kwa zaidi ya miaka 50 sasa.
Mwisho
CCM waache kufanya siasa nyepesi zenye ghiriba na kuhadaa
wananchi, ni wakati wa wanahandeni kuungana pamoja kuendelea kufanya mabadiliko
ya kukataa chama chenye serikali iliyoshindwa kuleta ya huduma ya maji.
Imetolewa na Mashuve Aroni
Mwenyekiti wa BAVICHA TANGA
0756 923 945
Source: Mtoi M. (Sept. 2013). Ukweli wa Handeni kuhusu wanachama waliokihama CHADEMA. Retrieved from Jamii Forums
No comments:
Post a Comment