Siku saba tangu Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (Nec), kumvua uanachama, Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki, Mkoa wa Mjini Magharibi, Mansour Yussuf Himid, kutokana na kukiuka miiko ya chama hicho, ameibuka jana na kukiponda chama hicho kuwa kimejaa siasa za chuki na ubaguzi. Huku akizungumza kwa umakini na kujiamini alisema, “ CCM kimejaa ubaguzi, siasa za chuki na kimeshindwa kusimamia misingi imara ya kutetea masilahi ya wananchi. Wazanzibari kataeni hali hii, wekeni tofauti za vyama pembeni, Zanzibar kwanza vyama baadaye. Tusimamie muungano wa heshima, haki na usawa.”
Himid ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar yenye wajumbe sita, alitoa kauli hiyo jana katika kongamano la wazi lililoandaliwa na kamati hiyo katika ukumbi wa Hoteli ya Bwawani na kuongozwa na mwanasiasa mkongwe ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati hiyo, Hassan Nassor Moyo. Katika hotuba yake ya dakika 46, Mansour ambaye kwa nyakati tofauti amewahi kuwa Waziri na Naibu Waziri wa Maji, Nishati, Ardhi na Mazingira, Waziri wa Kilimo, Waziri asiyekuwa na Wizara Maalumu na Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar, aliendelea kusimamia msimamo wa muundo wa muungano wa serikali tatu kwa kufafanua kuwa, “Muundo wa muungano wa serikali tatu ni wimbi kubwa halizuiliki tena.”
Source: butahe F., & Ussi T. (September 2013).Mansour: Viongozi CCM wanafiki, wamejaa chuki. Retrieved from Mwananchi
No comments:
Post a Comment