Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Wednesday, September 4, 2013

Kigwangalah awazulia jambo mawaziri

JIBU LA SWALI LA MBUNGE NZEGA


      MBUNGE wa Nzenga, Dk. Hamis Kigwangalah (CCM), amewatuhumu baadhi ya mawaziri na wabunge akidai wamehongwa na makampuni ya biashara ya pembejeo za kilimo ili kupitisha Muswada wa Sheria ya Vyama vya Ushirika nchini. Vyanzo vyetu kutoka ndani ya kikao cha wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichokuwa chini ya Uenyekiti wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, vilidai kuwa baadhi ya wabunge walimtuhumu Dk. Kigwangalah kuwa amehongwa na Apex ili apinge hoja ya serikali. Katika kikao hicho Dk. Kigwangalah alituhumiwa kuwa ni miongoni mwa watu ambao wamepewa tenda ya kusambaza pembejeo za kilimo kwa wakulima wa tumbaku nchini kupitia kampuni yake binafsi. Kutokana na mjadala huo kuwa moto, wabunge hao walilazimika kutoka na azimio la kuifuta Apex kama njia ya kunusuru kupitishwa kwa muswada huo wa sheria ya vyama vya ushirika.

      Kwamba, kutokana na tuhuma hizo kwa pande zote, ilimlazimu waziri mkuu kutumia busara ili kumaliza sakata hilo. Hali hiyo ilimfanya Dk. Kigwangalah kuomba nafasi ya kujitetea mbele ya kikao hicho, ambapo alisema kuwa katu hajawahi kuhongwa na wenye makampuni ya watu wanaosambaza mbolea kwa lengo la kuipigia debe Apex. Chanzo chetu kilidokezwa kuwa kutokana na ukali waliokuwa nao wabunge wengi wa CCM, kikao hicho kiliamua kumpa onyo Mbunge wa Mpanda Vijijini, Moshi Kakoso, kutokana na tuhuma zake alizozitoa bungeni dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB),Vita Kawawa, pamoja na Makamu wake, Said Nkumba. Viongozi hao wanadaiwa kuidhinisha mamilioni ya shilingi dhidi ya mkurugenzi mtendaji wake.

     Alipotafutwa kuelezea tuhuma hizo za kuhongwa kwa madai kuwa amepewa tenda ya kusambaza pembejeo kupia Mwenyekiti wa Apex, Moshi Kakoso, Dk. Kigwangalah alisema hatua ya Bunge kupitisha muswada huo wa sheria ipo siku madudu yatakuja kuibuka na dhambi itawarudia wabunge waliopitisha. Alisema katika kipindi cha miaka minne iliyopita kazi hiyo ilikuwa ikifanywa na TTB ambayo imeonekana kushindwa kazi, hasa baada ya Apex kujitoa na kuanza kujisimamia wenyewe. “Daima ninachotaka kusema ni kuwa mimi ni mfanyabiashara, hata kama ni kutajirika sikutajirika kupitia Bunge ila kwa kipindi kirefu nilikuwa nafanya biashara ya pamba lakini hili la kampuni yangu kupewa tenda na Apex si kweli na kama wao wana ushahidi waseme ni kampuni gani.

       “Niliapa mbele ya waziri mkuu na kikao cha wabunge wa CCM kuwa kama yupo mtu mwenye ushahidi mbele yangu na ajitokeze.
“Mbona kuna taarifa za baadhi ya mawaziri na wabunge kuhongwa ili waweze kupitisha muswada huu na kuifuta Apex? Huu ni ukoloni mambo leo, sasa unarejeshwa nchini kwa mlango wa nyuma,” alisema.

Source: Kaijage D. (Sept. 2013).Kigwangalah awazulia jambo mawaziri. Retrieved from Tanzania Daima

No comments: