Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Saturday, August 31, 2013

Wengi wafungwa kwa kutojua haki


      ASILIMIA 70 ya wafungwa nchini wamehukumiwa kwa kesi mbalimbali kutokana kutofahamu haki zao za kisheria na kukosa msaada wa kisheria. Takwimu hizo zilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika ya Watoa Huduma ya Msaada wa Kisheria Nchini (TANLAP), Christina Kamili, alipokuwa akizindua ripoti ya utoaji msaada wa sheria ya mwaka 2011/2012. Alisema hukumu hizo zilitokana na mshtakiwa kushindwa kujipambanua mahakamani na kutumia fursa za kisheria. Alisema sababu nyingine ni kwa mshtakiwa kushindwa kumudu kupata utetezi wa mwanasheria huku taratibu za kisheria za makosa ya jinai zikitaka usikilizwaji wa haki kwa kutoa fursa kwa mshtakiwa/washtakiwa kuwa na haki ya kupata usaidizi wa kisheria.

      Akizungumzia ripoti hiyo, Kamili alisema takwimu zinaonyesha watu 23,430 walipata huduma ya kisheria kwa mwaka huo katika masuala ya ardhi, mirathi, ndoa, unyanyaswaji wa kijinsia, malezi ya watoto na kazi huku kesi 11,302 zikimalizika na 15,698 zikiwa bado mahakamani. Mwenyekiti wa bodi ya TANLAP, Dk. Judith Odungu, alisema mambo muhimu yaliyojitokeza katika utafiti huo ni ukosefu wa ufahamu kuhusu haki za msingi na wajibu wa watu wanaoishi katika mazingira ya vijijini ambao unaweka pengo katika upatikanaji wa haki zao. Pia alisema uhaba au rasilimali fedha zisizotosheleza katika utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria unachangia utegemezi mkubwa wa kifedha kutoka kwa wafadhili usio endelevu.

Source: Joslah J. (August 2013).Wengi wafungwa kwa kutojua haki. Retrieved from Tanzania Daima

No comments: