Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Saturday, August 10, 2013

Wagonjwa Muhimbili wahaha


     MASHINE ya Magnetic Resonance Ination (MRI) inayotumika kupima magonjwa mbalimbali katika mfumo wa fahamu imeharibika kwa zaidi ya siku nne na kusababisha usumbufu mkubwa. Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumamosi, umebaini kuwa wagonjwa wengi waliohitaji huduma hiyo wameshindwa kuipata kutokana na kuharibika kwa kifaa hicho muhimu cha kupima na kutambua magonjwa mbalimbali katika ubongo, uti wa mgongo na kifua. Akizungumza kwa niaba ya mgonjwa wake, Joshua Shaka, alisema kuwa wamekuwa wakihangaika kutafuta huduma hiyo kwa siku nne mfululizo bila mafanikio baada ya kuelezwa kuwa mashine hiyo imeharibika. Alisema kuwa kuna umuhimu wa serikali kuangalia namna ya kuagiza mashine mpya kwa kuwa iliyopo imekuwa ikiharibika mara kwa mara. “Hii mashine sio mara ya kwanza kuharibika; unaweza kuja leo ukaambiwa inafanya kazi lakini baada ya muda mfupi inashindwa kuendelea na kazi …inawezekana ni kutokana na uchakafu,” alisema.

       Alisema kuwa mashine hiyo ndiyo inayotoa huduma kwa hospitali zote za serikali kwa jiji zima la Dar es Salaam hivyo hatua ya kuharibika mara kwa mara imekuwa ikisababisha kuwepo kwa mlundikano wa wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo. “Hata hiyo mashine ya CT SCAN inayosemekana ipo hivi sasa nayo haina filimu hivyo unapopigwa unashindwa kupewa majibu hapo hapo jambo linalozidi kumfanya mgonjwa azidi kuumwa zaidi maana anategemea aje hospitali apate huduma,” alisema. Tanzania Daima Jumamosi, katika uchunguzi wake, lilidhihirishiwa uharibifu wa mashine hiyo na baadhi ya wahudumu waliokutwa hospitalini hapo. “Mashine ni mbovu kama mnataka huduma labda mniache simu zenu kama itapona wiki ijayo nitawapigia ili muweze kumleta mgonjwa wenu kuliko mje tena mkute mashine haifanyi kazi mtakuwa mnamchosha mgonjwa wenu bure,” alisema mmoja wa wahudumu waliokuwepo. Ofisa uhusiano wa hospitali hiyo, Aminieli Aligaesha, hakupatikana baada ya ofisi yake kufungwa kwa muda mrefu, na hata alipotafutwa kwa njia ya simu yake ya kiganjani nayo iliita mara nyingi na kwa muda mrefu bila majibu. Hata hivyo Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamaja, alikiri kuharibika kwa mashine hiyo na kusema kuwa wamemaliza kukitengeneza jana na kwa sasa kinafanyakazi.

Source: Kangonga B. (August 2013). Wagonjwa Muhimbili wahaha. Retrieved from Tanzania Daima

No comments: