Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Saturday, August 10, 2013

Nagu: “Ni vigumu kuongoza watu maskini


      WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mary Nagu, amesema kuwa ni vigumu kuwaongoza watu maskini na wenye njaa. Nagu alisema hayo juzi jijini hapa wakati akifunga maonesho ya 20 ya Nanenane kanda ya kaskazini yaliyojumuisha mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara ambapo Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Nchini (TaCRI) iliibuka mshindi wa jumla. Waziri Nagu aliyaonya makampuni na watu binafsi kuacha kuzalisha pembejeo na zana feki za kilimo kwani hatua yao hiyo mbali ya kuwapa hasara wakulima lakini pia huwasababishia njaa. Alisema kuwa wazalishaji wa pambejeo na zana feki za kilimo wamekuwa wakiwaathiri wakulima kiuchumi na wakati mwingine kuwasababishia njaa kwa kuwa mazao hayaoti. Waziri Nagu aliwataka watumishi wote wa serikali wanaohusika na usimamizi na udhibiti wa pembejeo na zana hizo kufanya kazi zao kikamilifu ili kuwabaini na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaofanya udanganyifu.

       Aidha aliwataka viongozi kuhakikisha wanapanga mipango mizuri ya matumizi ya ardhi ili kuepuka migogoro ya ardhi inayojitokeza kwenye maeneo mengi baina ya wakulima na wafugaji na wakati mwingine husababisha baadhi ya wananchi kupoteza maisha. Waziri Nagu alitaka kila wilaya ichague vijana watano waliohitimu chuo kikuu ili wawezeshwe kwa mitaji na ardhi waendeshe shughuli za kilimo ili kusaidia kupata ajira na kubaki kwenye maeneo yao badala ya kukimbilia mijini. “Niwahakikishie Waziri Mkuu (Mizengo) Pinda na Rais wetu (Jakaya Kikwete) kwa pamoja wanaunga mkono suala hili, wakuu wa mikoa na wilaya hakikisheni mnawachagua vijana watano kila wilaya, waliohitimu vyuo vikuu tuwawezeshe mitaji na ardhi ili wabaki hukohuko vijijini na kupunguza kasi ya vijana wanaokimbilia mijini kutafuta ajira,” alisisitiza Nagu.

Source: Macha G. (August 2013).Nagu: “Ni vigumu kuongoza watu maskini. Retrieved from Tanzania Daima

No comments: