Kuna
taarifa zimewekwa hapa kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara, Zitto ataanza safari ya
kuimarisha chama katika mikoa 5 hapa nchini na kwamba inatokana na yeye
'kujitenga' na ziara inayoendelea hivi sasa ya Mabaraza Huru ya Katiba Mpya,
kukiwa na timu mbili, chini ya viongozi wakuu wa kitaifa, Mwenyekiti Freeman
Mbowe na Katibu Mkuu, Dkt. Willibrod Slaa, ambapo kila timu inatumia usafiri wa
chopper! Wana
CHADEMA wawe makini na upotoshaji au hila za kuwaondoa kwenye focus ya suala la
Katiba Mpya, hasa ambapo kwa sasa chama kinakusanya maoni ya wanachama na
wapenzi wake juu ya Rasimu ya Katiba Mpya, kwenye mikutano ya hadhara
inayoendelea nchi nzima.
Maandalizi
yaliyopo kwa ajili ya ziara ya Naibu Katibu Mkuu, si kwa ajili ya mikoa 5 kama
ilivyopotoshwa, bali ni mikoa 3 ambayo ndiyo inayounda Kanda ya Magharibi,
ambapo yeye akiwa kiongozi mwandamizi wa chama kutoka kanda hiyo, pia kama
mbunge wa eneo husika, pamoja na viongozi wengine wa chama katika mikoa ya
Katavi, Kigoma na Tabora, anawajibika kuhakikisha kanda hiyo inatimiza majukumu
yake kwa kadri ya malengo na maelekezo ya chama, yaliyoamuriwa kwenye vikao. Ziara ya
Naibu Katibu Mkuu, kama ilivyo ziara za kichama za viongozi wengine huwa
zinatolewa taarifa rasmi. Wakati ukifika, baada ya kuwa taratibu zote, ikiwemo
kupitishwa katika vikao na 'modes of operandi' kuwekwa, umma utajulishwa na
kupewa taarifa ya ziara.
Hapa
chini ni response ya Naibu Katibu Mkuu Zitto juu ya taarifa hizo zenye
upotoshaji na bila shaka zikilenga kuwaondoa wana CHADEMA kujikita kujadili
masuala ya msingi ambayo chama chao, kwa niaba ya Watanzania, kinapaswa
kuyasimamia katika ngazi mbalimbali kwa ajili ya mstakabali wa nchi yetu na
jamii nzima ya Watanzania kwa ujumla. Moja,
sijajitenga na ziara ya chopa. Mimi ni Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, kamati hii
inasimamia mahesabu ya Serikali. Ziara inafanyika kipindi cha kamati za Bunge
na hivyo sikuweza kushiriki kwani ni hatari mno kuacha PAC chini ya wabunge wa
CCM peke yake.
Leo kamati inahoji Wizara ya Elimu yenye madudu kibao, Hazina
yenye kukusanya mapato yote ya Serikali na ratiba nzima nitawasilisha hapa.
Haya yote uongozi wa chama unajua. Ni mgawanyo tu wa majukumu. Hata hivyo
nimeshiriki kuandaa mikutano katika mkoa wa Kigoma na gharama zote za maandalizi
nimetoa mimi. Hata gari anayotumia mwenyekiti huko Kigoma ni gari yangu. Kusema
nimesusa ni uzushi sana wenye lengo la kuleta mgogoro kwenye chama.
Pili,
mimi ni mbunge kutoka Kanda ya Magharibi. Kila kanda imepewa wajibu wa
kujiimarisha kichama. Nimekuwa nilifanya hivi toka kanda zimeundwa. Kuanzia
mkutano wa mwanzo nimekuwa nikitimiza wajibu wangu wa kuhakikisha kwamba kanda
ya magharibi inakuwa imara kichama. Nimefanya ziara kadhaa mkoa wa Kigoma na
mkoa wa Tabora. Hivi sasa kanda zote zinapaswa kufanya uchaguzi wa ndani ya
chama. Nimeamua kuanzi tarehe 20 Septemba (mara baada ya Bunge mkutano wa 12
kumalizika) kuanza ziara ya kanda ya magharibi kuchochea ujenzi wa chama
kuanzia matawi ili tuweze kuendana na ratiba ya uchaguzi. Ziara hii itafuata taratibu
zote za chama na sijaamua naifanya na nani maana maafisa wa chama wanapingiwa
na katibu Mkuu.
Ninasikitika
sana kwamba kumekuwa na tabia za kuchonganisha viongozi wa chama bila sababu
kwenye mitandao ya intaneti. Kwa mtu anayeipenda chadema hawezi kufurahi mambo
haya. Mimi
kama Zitto siwezi kufanya jambo lolote la kuathiri chama changu ambacho
nimeshiriki kukijenga kwa kadiri ya uwezo wangu. Ninaomba pia watu wengine
watumie muda zaidi kuunganisha viongozi badala ya kuwagwa. Tunahitaji sana
umoja na mshikamano wa dhati
Tumaini Makenu
Kurugenzi ya habari CHADEMA
No comments:
Post a Comment