Na Ashakh (Kiongozi)
Ikumbukwe miaka miwili
nyuma ndani ya chama tawala CCM kuliibuka kundi lenye mzozo na kundi jengine
kuputia dhana na kauli mbiu ya “Kujiva Gamba”. Kauli hii ilitokana na lile
kundi la viongozi waliojiona kuwa ni wasafi mbele ya kundi la viongozi
walioshukiwa kujihusisha na mambo rushwa. Uhasama ukajengeka
miongoni mwao hivyo kutakiwa wale wote wanaojihusha na vitendo vya ufisadi
kujchukuliwa hatua ya kuvuliwa nyadhifa za uongozi na kufukuzwa uanachama.
Kama vile unayebeba
kilo 100 za usufi, dhana ya kujivua gamba ndani ya CCm haikuweza kutekelezwa.
Licha ya kuonekana wepesi wake, ugumu ulikuwa umezidi na kuumiza migogo ya
viongozi na wale wote walizaa dhana hii. Leo hii fununu
zimetanda kutaka utekelezaji wa dhana ile, kwa baadhi ya viongozi wa CCM
Zanzibar kupendekeza baadhi ya wananchama wao wavuliwe gamba. Tofauti kidogo
sababu kuu ya kuvuliwa gamba na pale mwanzo. Mara hii ni kwa wale wanachama
waliotumia fursa ya kuwataka Watanzania wote washiriki na watowe maoni yao
katika upatikanaji wa katiba mpya ya Tanzania.
Hii ni aibu, kwani kama
mwananchi wa Tanzania bila ya kujali itikadi ya chama, kutoa maoni ni haki ya
kila mtu kwa mujibu wa sheria. Vipi leo kuwe na fukutu la kufukuzwa uanachama
kwasababu tu mawazo yako yako kinyume na mawazo ya wengine. Hivi kweli CCM inaweza
kujivua gamba? Vipi kwa wale wengine waliokuwa na mawazo sawa na wanachama
wanaofukuzwa uanachama. Tukichukulia mifano kama vile Jaji Joseph Warioba, Dr
Salim Ahmed Salim, Mzee Hassan Nassor Moyo, na wengineo wote hawa ni CCM nao
hawakubaliani na Ilani ya CCM kupatikana katiba mya, jee na wao watafukuzwa
uanachama?
Yataka
ujasiri “Kujivua Gamba”
No comments:
Post a Comment