Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), leo kinaanza rasmi kuendesha Mabaraza ya Katiba, ambapo wananchi
wote watashirikishwa kujadili na kutoa maoni yao juu ya Rasimu ya Katiba Mpya,
kwa njia mbalimbali kama ifuatavyo;
1. Mikutano ya hadhara, itakayoanza
leo katika maeneo mbalimbali ya nchi, ikiongozwa na timu mbili za
viongozi wakuu, Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dkt. Willibroad
Slaa. Mikutano hiyo
itafanyika nchi nzima. Ratiba ya mikutano yote, itatolewa kwa umma, kupitia vyombo vya
habari (mainstream & social media).
2. Kutuma ujumbe mfupi kwa simu.
Mwananchi anaweza kutuma maoni yake ya Katiba Mpya kupitia simu ya
mkononi, kwenye NAMBA HII YA SIMU; 0789 24 82 24.
4. Mitandao ya kijamii, mf; Jamii
Forums, facebooks, twitter, group emails, k.m mabadiliko, wanabidii n.k,
utaratibu wake utatolewa kwa umma, kupitia vyombo vya habari, ikiwa
ni pamoja na
kuwekwa hapa, namna ambavyo Watanzania wote watashiriki kutoa maoni yao kwa njia
hii.
Tumaini Makene
CHADEMA Senior Information(Press)
Officer
0752 691569/ 0688 595831
No comments:
Post a Comment