Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Saturday, August 24, 2013

NEWS ALERT: CHADEMA yaisambaratisha CCM uchaguzi wa kijiji Kondoa, ni jimboni kwa Juma Nkamia


Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimezidi kuonyesha umwamba wake kwa chama cha Mapinduzi baada ya kukibwaga vibaya kwenye uchaguzi wa kijiji Kondoa Kusini.

Uchaguzi huo ulifanyika jana katika kijiji cha Mlongia Kata ya Jangalo.Katika matokeo yaliyotangazwa muda mfupi uliopita mgombea wa Chadema ameibuka mshindi kwa kupata kura 184 dhidi ya 96 za CCM.Mgombea wa CUF ameambulia kura 9.Huu ni ushindi wa asilimia 64% kwa Chadema.

Mbunge wa Jimbo hilo ni Juma Nkamia wa CCM ambaye mara kadhaa amekuwa akiibeza na kuishambulia Chadema awapo bungeni.

Huu ni ushindi mkubwa kwa wanamageuzi kwani kijiji cha Mlongia ni kati ya vijiji vilivyoko ndani kabisa mkoani Dodoma.

Molemo/JF

No comments: