- Awasuta wanaotaka Serikali Mbili
- Awashangaa wanaotaka Zanzibar iendelee kuwa manispaa
- Mwanasheria Mkuu SMZ: Serikali Mbili zitavunja Muungano
- Asema kutokuwepo Serikali ya Tanganyika ndio kero
Kuu ya Muungano
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi wa Zanzibar
leo amesema lengo la kuandikwa kwa Katiba Mpya si kuyafanyia Marekebisho katiba
iliyokuwepo sasa bali ni kandika Katiba Mpya katiba ambayo itakuwa Muarubaini
kwa kero za Muungano na Muungano wenyewe. Mwanaseheria Mkuu liyasema hayo
leo asubuhi alipokwa akifunguwa Baraza la Katiba la Vyuo Vikuu liliondaliwa na
ZAHILFE Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Zanzibar liliofanyika katika
Ukumbi wa Salama Hal Bwawani. Alilisifu Baraza hilo na kusema kuwa ni
Baraza la Vijana wasome na kuwasifu Vijana kwa ile sifa yao kubwa ya kuleta
mapinduzi katika jamii yeyote.
Alimtaja kijana Sir King ndie waliosababisha
Zanzibar iiteme Tanganyika mwaka 1895 Ogast na Tanganyika kuangukia katika
mikono wa Wajerumani. Na kumtaja Gerald Pota alietumwa na Waingereza kuja
kuunda Serikali na kumpangia Mfalme mshahara ambako alikuwa akilipwa paund 250
kwa mwaka. Msingi wa Muungano wa Tanzania ni kuungana kwa Nchi mbili huru
Tanganyika na Zanzibar lengo la kuungana kwa nchi mbili hizi ni kufanya mambo
yao pamoja na kupata faida zaidi na sio Nchi moja kuitawala Nchi nyengine
alisema, hukua akiendela kusema:
Zanzibar si mkowa wala wilaya, Zanzibar ni
Nchi, katika Muungano tulikubaliana baadhi ya mambo kufanya pamoja na sio
Zanzibar kuwa Jimbo la Tnganyika. Alisema duniani kuna miungano mingi
mizuri akiutolea mfano Muungano wa Uswis ambao una Serikali 24 na ule wa
Muungano wa Maerkali wenye Serikali 52 na kusema kuwa ni uongo kuwa Serikali
Tatu zitavunja Muungano na kusema Serikali Mbili ndizo zitakazovunja Muungano,
na hata Muungano wa Serikali Tatu ukivunjika si kioja. Serikali Tatu
hazitovunja Muungano Serikali Mbili ndizo zitakazo vunja Muungano.
Alisema Uruhani wa Serikali ya Tanganyika ndio kero kubwa ya Muungano na
Serikali tatu itairudisha Serikali ya Tanganyika ambako kero kubwa itakuwa
ishatatuliwa. Aliitaja Sheria ya Kuanzishwa na Bank Kuu ya Tanzania kuwa
aliisaini Karume mwenyewe lakini Karume alipoona mapungufu ya Seria hiyo ndio
maana akaanzisha PBZ. Aidha alisema kama Zanzibar inataka kuishtaki TFF
itashinda na TFF haitokuwemo FIFA kwani TFF haiwakilishi Tanzania kama
ilivyokuwa ZFA ilivyokuwa haiwakilishi Tanzania.
Hivi hatuoni haya kubakia hivi hivi kuwa Manispaa
wakati Zanzibar ilikuwa Empire alihoji Mwanasheria Mkuu na kuendelea kusema
hivi tutamuamini vipi mtu ambae leo anasema Zanzibar si Nchi atakapokuwa Rais
wa Tanzania ambao Zanzibar haitokuwa na Mamlaka atasema Zanzibar ni jimbo la
Tanganyika na kumalizia kusema wengi wa Watanganyika wanachuki na
Zanzibar. Aliwataka wanafunzi hao kuzungumzia mambo ya Muungano na kutaka
kuwe na usawa “Bila ya kuwa na usawa katika Mungano huu huo si Muungano bali ni
ukoloni” alisema, na kutaka kuwe na mfumo wa usawa katika Baraza la Mawaziri na
Bunge na kuwe na makubaliano ya thuluthi mbili kila upande katika kupitisha
sheria na kuengezwa au kupunguzwa mambo ya Muungano.
Alisema katika Muungano wa Serikali Tatu ni
lazima Rasilimali zitumike kwa Usawa na sio kama hivi sasa Tanganyika
inavyotumia Rasilimali za Muungano wao peke yao katika kusoma na kuinyima
Zanzibar. Tume ya Pamoja ya Fedha haijaanza kazi mpaka leo, na katika
Muungano kuna mapato ya Muungano na Matumizi ya Muungano na Mapato ya Muungano
siku zote huwa mengi ambako Tnganyika hawataki tugawane. Alisema si kweli
kama Muungano wa Serikali tatu una harama bali Muungano wa Serikali Mbili ndio
wenye gharama na Zanzibar ndio inaharamika zaidi, aliwataka viongozi wawe
wakweli na waache kuwapotosha wananchi.
Aliwaonya Wazanzibar kuwacha kulumbana na badala yake
kukaa pamoja kuidai nchi yao. Alisema Serikali ya Umoja wa Kitaifa
iliundwa ili kuondowa tofauti kwa Wazanibar na kusema kuwa kuundwa kwa Serikali
ya Umoja wa Kitaifa ni kuala gumu kuliko mabadiliko ya Muungano. Alisema
Wanaotaka Seriakali Mbili hoja zao hazina msingi na hakuna haja ya kubakia
kwenye Serikali mbili na wengi wanaotaka Serikali Mbili wanalinda maslahi yao
ya kidunia. Hoja yangu nawataka wanaotaka Serikali Mbili na Wanaotaka
Mkataba wakae pamoja wajadiliano Mfumo wa Muungano wa Serikali Tatu mfumo ambao
utakuwa na Mslahi na Zanzibar.
Awali Mwenyekiti wa ZAHILFE alikanusha taasisi yake kuandaa kungamano la
tarehe 6 mwezi wa 7 lililofanyika Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kingeni na
badala yake kongamano hilo liliandaliwa na Mkowa wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu
vywa CCM na kusema Taasisi yake haina mafungamano na chama chochote cha
siasa. Kongamano hilo lilianza na Wimbo wa Taifa wa Zanzibar na
lilihudhuriwa na baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi. Marais 10 wa
Serikali za Wanafunzi waliochangia katika Kongamano hilo walitaka Zanzibar
yenye Mamlaka Kamili na Usawa Katika Muungano.
Source: Salim S. ( August 2013). MWANASHERIA MKUU SMZ ” SERIKALI 2 NI KUVUNJA MUUNGANO. Retrieved from Mzalendo net
No comments:
Post a Comment