Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Tuesday, August 6, 2013

Mbunge wa CCM Nzega, Hamis Kigwangala: Sitompa kura ya uraisi Lowassa 2015



  Mbunge wa Nzega Hamis Kigwangalla amesema hawezi kumpa kura yake Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli Mheshimiwa Edward Lowassa endapo jina lake litajitokeza kama mmoja ya wagombea urais, ni kauli ya Kigwangalla akijibu swali aliloulizwa na Mtangazaji Fina Mango katika kipindi cha Makutano kuhusu vuguvugu la urais 2015 linaloendelea ndani ya CCM juu ya mgombea urais ambapo Edward Lowassa ni kati ya wanaotajwa sana kama wagombea hasa katika mitandao ya kijamii.

      “Sitompa kura Mheshimiwa Edward Lowassa kwa sababu za msingi tu, kwamba ninakipenda chama changu na nina hakika chama changu kikija na mgombea kwenye uchaguzi mkuu 2015 ambaye ana historia ya kuhusishwa na mambo machafu kama yale ya Richmond, Dowans ambayo unayasema, hapa tunaweza kupata tabu sana kuomba kura kwa wananchi, lakini pia tutakuwa tumewapa hoja wapinzani wetu ya kusema tunalea ufisadi, tunaubembeleza ufisadi kwa mikono miwili’ Kigwangalla

    Kwenye sentensi nyingine Kigwangalla amesema Tanzania aihitaji rais asiyeweza kusimamia ukweli ambapo kuhusu ishu ya dowans amesema haoni tatizo la mitambo hiyo isipokuwa uamuzi uliotumika katika upatikanaji wake. Kwenye hii interview, Kigwangalla alitangaza nia ya kugombea urais mwaka 2025 na kusema 2015 anaona bado ni mapema kwake kwani anaamini watanzania bado hawajamjua Hamis Kigwangalla ni mtu wa aina gani.

No comments: