Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Sunday, August 11, 2013

Mbowe alia na Katiba kutoa fursa kupitia upya mikataba




    Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema chama chake  kitapigana kufa na kupona kwenye bunge la katiba  mwezi ujao, kuhakikisha, katiba hiyo inatoa fursa ya kupitiwa upya mikataba yote ambayo serikali imeingia na wawekezaji. Mbowe na wabunge wenzake 12 wa chama hicho, wapo katika jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro,  kukutana na kuzungumza na wananchi masuala mbalimbali ya kitaifa ikiwamo rasimu ya katiba mpya, kuimarisha chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadili utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Alisema bila ya Chadema kufunga kibwebwe katika kudai mambo ya msingi kwa ajili ya nchi mambo ya msingi ikiwamo suala la rasilimali za wananchi ambazo viongozi wamekuwa wakiingia mikataba bila wawakilishi wao kushirikishwa au kujua ni tatizo ambalo hawatalifumbia macho .

       Mbowe ambaye ni Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni katika safari hiyo anayotumia helikopta, alitoa mfano shamba la TPC kwa kusema kuwa tangu liwekezwe hakuna anayejua  mwekezaji analipa Shilingi ngapi, wala kilichoandikwa kwenye mkataba huo, ambao umempatia mwekezaji huyo eneo kubwa la shamba pamoja na maji huku wananchi wakitaabika kwa uhaba wa ardhi. “Hatuwezi kuangalia mali yetu ikienda na wananchi wanataabika tukipata katiba mpya lazima mali zote zilizochukuliwa na wawekezaji  mikataba irudiwe na iweke hadharani mwekezaji kama huyu wa TPC aliuziwa shamba hilo na nani na kwa shilingi ngapi,”alisema. Hata hivyo katika hatua nyingine Mbowe alisema kuwa wazee wa Tanzania akiwamo Mwalimu Julius Nyerere walipigana kuwaondoa makaburu weupe na hivyo Chadema wanafanya kazi ngumu kumuondoa kaburu mweusi ili watoto wanaokuja waweze kufaidi rasilimali zilizopo nchini.

     Akizungumzia suala la maadili kwa viongozi, alisema kuwa katiba ambayo kwa sasa inafanyiwa mabadiliko imetumiwa vibaya na viongozi walioko madarakani kwa kuwalimbikizia wananchi kesi pamoja na kutowachukulia hatua viongozi wanaoiba rasilimali zao za umma. Alisema kuwa magereza nyingi wafungwa  wanaotumikia adhabu ni wale wezi wadogo wadogo huku viongozi walioiba mabilioni wakiendelea kufurahia maisha uraiani. Kwa Upande wake Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, alisema kuwa kama kuna kiongozi wa upinzani ambaye akifa CCM watafanya sherehe ni pamoja na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe.

      Alisema kuwa Mbowe amekuwa akifanya kazi ngumu, ambapo alisema mafanikio makubwa ambayo Chadema inayo ikiwamo kuwa na wabunge wengi vijana ikiwamo yeye imetokana kwa kiasi kikubwa na mchango wa Mbowe. Miongoni mwa Wabunge waliopo kwenye Ziara hiyo ni pamoja na Ezeckiel Wenje, Peter Msigwa, Joshua Nasari, Lucy Owenye, Grace Kiwelu, Joseph Selasini, pamoja na madiwani wa Chadema kutoka Moshi Manispaa na Hai.


Source: Mush G. ( August 2013).Mbowe alia na Katiba kutoa fursa kupitia upya mikataba. Rtreieved from Ippmedia/Nipashe

No comments: