“Katibu mkuu atawasili Lushoto na kufanya mkutano wa hadhara uwanja wa RRM saa mbili asubuhi, Handeni mjini saa 5.30 asubuhi, Korogwe Mazoezi saa 7.30 nchana, Muheza saa 9.30 uwanja wa CHADEMA Square na mkutano wa mwisho Tanga Jiji saa 11. 40 jioni,” alisema Bahweje. Katibu huyo alitoa wito kwa wananchi kuhudhuria mikutano hiyo katika maeneo hayo na kumsikiliza ili kupata misingi halisi ya mikutano hiyo. Sambamba na hayo, alieleza chama hicho ngazi ya mkoa kinaendelea na mikutano ya hadhara na ya ndani kwa kuanzia wilaya ya Korogwe kwa lengo la kuelezea mkakati wa CHADEMA. Alisema mikutano hiyo inafanyika katika vijiji vya Masange, Mngwasa na Lutindi vya kata ya Lutindi na kuendelea katika kata ya Bungu, jimbo la Korogwe vijijini.
Source: Kilindi E. (August 2013).Dk. Slaa kuunguruma Tanga Alhamisi. Retrieved from Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment