Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM) iliyomalizika leo imejadili kwa kina Masuala mbalimbali
likiwemo pendekezo la Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Magharibi - Zanzibar la
kumvua uanachama Ndugu Mansoor Yussuf Himid (pichani), Mjumbe wa Baraza la
Wawakilishi wa Kiembesamaki.
Baadhi
ya tuhuma za Ndugu Mansoor Yussuf Himid ni pamoja na:-
1.
Kushindwa kusimamia malengo ya CCM na kutekeleza masharti ya uanachama.
2.
Kushindwa kutekeleza wajibu wa mwanachama na kukiuka Maadili ya Kiongozi wa
CCM.
3.
Kuikana Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010-2015 na kuisaliti CCM.
Baada
ya kujiridhisha vya kutosha na tuhuma dhidi ya Ndugu Mansoor Yussuf Himid,
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) imeridhia uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM
Mkoa wa Magharibi Zanzibar wa kumfukuza uanachama. Kwa uamuzi huo wa kumvua
uanachama wa CCM Ndugu Mansoor Yussuf Himid, yeye kwa sasa sio Kiongozi tena wa
CCM.
Imetolewa
na:
Nape
Moses Nnauye,
KATIBU
WA
NEC ITIKADI NA UENEZI CCM TAIFA
26/08/2013
No comments:
Post a Comment