MSAJILI wa vyama vya Siasa, John Tendwa, hana uwezo
wa kuvifuta vikundi vya ulinzi na usalama vilivyoanzishwa na vyama hivyo, kwa
sababu aliruhusu vianzishwe. MTANZANIA Jumatano linaripoti. Msajili Msaidizi wa vyama vya siasa, Sisty Nyahoza,
ameliambia gazeti hili mwishoni mwa wiki katika mahojiano maalumu yaliyofanyika
ofisini kwake Dar es Salaam, kuwa sheria ya sasa kuanzishwa kwa vyama vya siasa
haimpi mamlaka Msajili wa vyama vya siasa kuvifuta vikundi hivyo.
Alisema, ingawa Msajili wa vyama vya siasa, Tendwa,
amekuwa akitoa tishio la kuvifuta vyama vya siasa hasa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), ambacho kimetangaza kusudio la kuanza kutoa mafunzo ya
ukakamavu kwa kikundi chake cha ulinzi na usalama cha Red Brigade, amekuwa
akipata kigugumizi cha kutekeleza adhabu hiyo kutokana na kubanwa na sheria. Nyahoza alisema ofisi yake baada ya kubaini hilo,
imeanzisha mchakato wa kuifanyia marekebisho sheria hiyo ili iwe na adhabu
zinazoweza kutekelezwa kwa urahisi kwa vyama vinavyokiuka misingi ya kuanzishwa
kwake bila kuathiri wananchi. “Adhabu iliyopo katika sheria hii ni kwamba, iwapo
chama kikiendelea kutoa mafunzo ya ukakamavu kwa vikundi hivi vya ulinzi ni
kukifuta chama, adhabu ambayo ni kubwa na ipo tu ndiyo maana utekelezaji unakua
hafifu.
“Ni sawa na kusema nchi ingekuwa na adhabu moja tu
ya kifo kwa kila kosa, ina maana watu wengi sana wangeuawa, ndiyo maana
tumekuwa tukiishia kubishana na vyama kwa sababu hakuna adhabu mbadala,”
alisema Nyahoza. Alipoulizwa iwapo Ofisi ya Msajili iliruhusu
uanzishwaji wa vikundi hivyo, alikiri jambo hilo, hata hivyo alieleza kuwa
ruhusa hiyo iliambatana na katazo la kutoa mafunzo ya ukakamavu. Alisema suala la ulinzi ni suala muhimu sawa na
kutoa ulinzi binafsi kwa mtu au kwenye taasisi nyingine, lakini kwa upande wa
vyama ulinzi wake unakuwa wa kipekee kwa sababu vyama ni taasisi kubwa
inayojumuisha idadi kubwa ya watu.
“Ibara ya 20 ya Katiba kifungu cha tisa cha vyama
vya siasa, tunaona kuwa vyama ni taasisi, kutokana na unyeti wake vimekuwa na
chombo maalumu kama hivyo vikundi. Alipoulizwa kuhusu malalamiko yanayoelekezwa kwenye
kikundi cha Green Guard cha CCM, kupewa mafunzo ya kijeshi na wahitimu
kutunukiwa vyeti alisema Tanzania ni nchi kubwa hivyo Msajili hawezi kufuatilia
kila tukio.
Source: Mushi G.
(July 2013).Tendwa hana ‘meno’ kwa Chadema. Retrieved from Mtanzania
No comments:
Post a Comment