Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), kimekosoa pendekezo linalotaka uteuzi wa Jaji Mkuu kuidhinishwa na Bunge, kwa madai kuwa kitendo hicho kinaweza kukandamiza mhimili wa mahakama. Katika moja ya mapendekezo yake, Tume ya Mabadiliko ya Katiba imetaka uteuzi wa Jaji Mkuu na msaidizi wake ufanywe na Rais kisha kuthibitishwa na Bunge. Rais wa TLS, Francis Stola alisema licha ya tume hiyo ikufanya kazi nzuri, hatua ya kutaka Jaji Mkuu aidhinishwe na bunge ni sawa na kuweka mhimili mmoja chini ya mhimili mwingine, jambo ambalo ni hatari kwa mustakabali wa taifa.
Stola alisema mapendekezo hayo ni jambo linalopaswa kutoungwa mkono, kwani linaweza kubinya uhuru na mamlaka zinazopaswa kuwa ndani ya mahakama. “Siyo jambo la busara hata kidogo Jaji Mkuu akichateuliwa na rais aende bungeni athibitishwe… hakuna kitu kama hicho, katika hili tume imekosea,” alisema Stola. Alisema uteuzi wa Jaji Mkuu na msaidizi wake halipaswi kuachwa mikononi mwa Rais, kwani taasisi ya Urais ni moja ya mihimili ya dola ambayo utendaji wake unasimamiwa na chombo kingine .
Source: Njogopa G. ( June 2013).Wanasheria wapinga Rais kuteua Jaji. Dar. Retrieved from Mkuu. Mwanchi
No comments:
Post a Comment