Wenzangu wanabodi, hususan wale waliberali, turudini kwenye ile hoja nyingine, maana mnataka kutumia 'kombora' la uliberali kama exit ya zile tuhuma nyeti zinazowakabili CUF na hasa mwenyekiti wenu na mgombea urais wa maisha, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba, kuwa;
1. Ni washirika wakubwa wa CCM kiasi mlijitoa mhanga, mkaligawanya taifa kwa misingi ya udini, ili CCM inusurike kuondoka madarakani iendelee kutawala.
2. Profesa Lipumba ni kati ya viongozi wa siasa wanaopaswa kuogopwa kama ukoma hapa nchini kutokana na kuwa na malengo ya kuwagawa Watanzania (wanaopendana kama ndugu) katika misingi ya imani za dini, hasa uislamu na ukristo. Inaonekana hata hatambui haki za watu wenye imani za dini zingine tofauti na hizo mbili na wapagani.
Ni mtu hatari sana huyu!
Lakini katika hali inayoonesha au kudhihirisha kumkoma nyani gidari...Tume ya Katiba Mpya, kupitia rasimu yake ya juzi, imepigilia msumari, hasa katika ibara ya 75(h)...
Ibara hiyo inayozungumzia sifa za mtu kuwa rais inasema;
Mtu atakuwa na sifa ya kuchaguliwa kushika nafasi ya kushika madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, ikiwa;
(h) Sera ZAKE au sera za CHAMA CHAKE, si za mrengo wa kuligawa taifa kwa misingi ya ukabila, udini, rangi au jinsia.
Wandugu wangu, hapo kwenye herufi kubwa msisitizo ni wa kwangu. Lakini hapa CUF ambao siku za hivi karibuni wameskikika wakililia 'utamu' wa kuwa mojawapo ya vyama vya upinzani, wakati keki yao walishaila baada ya kuamua kuungana na CCM kisirisiri kwenye uchaguzi mkuu kama alivyotoboa Profesa Lipumba kwenye ule mkanda wake wa udini na wakaungana na CCM kwanza sirini, kisha hadharani huko Zanzibar, hawachomoki.
Hadi tunavyozungumza hapa, si CUF wala Profesa Lipumba waliotoa hoja za maana juu ya ule mkanda wa video unaomuonesha Prof mzima akifanya kazi ambayo hata mtoto wa chekechea, akisimuliwa atasema 'hakuna maana ya kwenda shule, kama elimu haijamsaidia hata huyu profesa...kuwagawa watu...kwa udini'.
Atashindwa nini kutugawa kwa ushia, sunni, ukabila, kisha maeneo!
Tunashukuru watu wa tume, katika eneo hili, hakuna Mtanzania mpenda nchi yake, atapingana nanyi hapo. Ingawa kunasikika minong'oni kuwa Profesa na watu wake watakataa, maana ndiyo uchochoro wanaotaka tena kuutumia kuibakisha CCM madarakani, maana wao kama wao, hawawezi kushinda. Wanajua.
Watanzania wote, bila kujali tofauti zetu zingine tuiunge mkono hii ibara hasa hicho kipengele.
Wote wataanguka anguko moja, maana wako pamoja.
No comments:
Post a Comment