SERIKALI
imekiri kuwapo kwa msongamano wa wafungwa katika magereza yote nchini likiwamo
Gereza la Ngudu. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame
Silima, alisema jana bungeni kuwa ili kukabiliana na tatizo hilo Jeshi la
Magereza kupitia bajeti linayopewa na serikali limekuwa likiyatatua kwa awamu,
kwa kuyafanyia ukarabati magereza yaliyopo, kukamilisha na kujenga magereza
mapya katika wilaya ambazo hazima magereza. Alisema lengo ni kuongeza
nafasi za kuhifadhi wafungwa magerezani.
Naibu waziri alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu,
Leticia Nyerere (CHADEMA), ambaye alitaka kujua serikali itarekebisha lini
jambo hilo na msongamano katika magereza hasa Gereza la Ngudu ili kuepuka
ukiukwaji wa haki za binadamu.
Source: Chademablog
No comments:
Post a Comment