Wizara za Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia zitawasilisha bajeti zao wiki hii kwa mwaka 2013/14 huku Watanzania wakisubiri kupata majibu kadhaa baada ya kubainika watendaji wake kushindwa kutimiza wajibu wao ipasavyo. Kutokana na wizara hizo kuwa tegemeo kubwa la Watanzania, katika siku za karibuni wananchi na wabunge wamekuwa na mjadala wa kutaka mawaziri kuwabika kwa kushindwa kutatua matatizo yanayowakabili wananchi kupitia wizara zao.
WIZARA YA ELIMU
Shinikizo la kutaka Dk. Shukuru Kawambwa ajiuzulu liliibuka baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012 ambayo yalikuwa mabaya na watahiniwa asilimia 60 walipata alama sifuri. Shinikizo la kutaka Dk. Kawamba ajiuzulu liliibuliwa bungeni Februari mwaka huu na mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia alipowasilisha hoja binafsi kuhusu udhaifu katika sekta ya elimu. Hoja hiyo ambayo ilizua malumbano makali, Mbatia alibainisha kuwa sekta ya elimu ina udhaifu mkubwa kuanzia kwenye sera, mfumo rasmi wa elimu, mitalaa, mihtasari na udhaifu katika vitabu vya kiada na ziada.
Kabla suala hilo halijapoa, kukaibuka suala la matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ambayo nayo yalimweka katika wakati mgumu Dk. Kawambwa aliposhinikizwa kujiuzulu. Ni katika matukio hayo, shinikizo la Dk. Kawambwa kutakiwa ajiuzulu liliibuka tena kwenye kikao cha wabunge wa CCM na Rais Jakaya Kikwete. Hata hivyo, serikali baada ya kuona kuna tatizo katika suala hilo iliunda tume ambayo ilipendekeza kufutwa kwa matokeo ya awali kwa kuwa mfumo wa upangaji alama uliotumika haukuwa umeshirikisha wadau.
Hali kadhalika upungufu wa walimu hasa wa sayansi na hisabati, kutopandishwa madaraja kwa walimu na malimbikizo ya madai ya walimu ambao wanatajwa kuwa wamechangia matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka jana ni miongoni mwa mambo yatakayolitikisa Bunge.
WIZARA YA MAWASILIANO
Watanzania wanasubiri majibu kutoka kwa wizara hiyo kwani tulipoingia katika mfumo wa dijitali kutoka analogi kumezua malalamiko megi ya wananchi wanaokosa haki ya kupata habari.Wamiliki wa vituo vya televisheni wameiomba serikali kuongeza muda wa kuhamia digitali kwa kuwa wamekuwa wakipoteza watangazaji hivyo kuviweka kwenye hatari ya kushindwa kujiendesha.
Tatizo la usajili wa simu ambalo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imeweka mwisho ni Juni 30 limekuwa na malalamiko mengi kwasababu tangu zoezi hilo limeanza wapo baadhi ya watu wanaendelea kutumia laini zisizosajiliwa. Suala la kutolipa kodi kikamilifu kwa kampuni za simu, ununuzi wa kifaa cha kufuatilia mwenendo wa mapato wa kampuni hizo na kukosekana kwa mawasiliano maeneo vijijini
Source: Ippmedia (June 2013). Ni wiki ya kukaangwa Kawambwa, Mbarawa. Retrieved from Ippmedia/Nipashe
No comments:
Post a Comment