Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Thursday, June 6, 2013

Mbunge ahoji upatikanaji wa vitambulisho vya taifa


JIBU LA SWALI LA MBUNGE MBOZI MAGHARIBI


David Silinde,  Mbunge, CHADEMA
     MBUNGE wa Mbozi Magharibi, David Silinde (CHADEMA), ameitaka serikali ieleze ni lini itamaliza zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya taifa. Silinde alitoa kauli hiyo bungeni jana alipokuwa akiuliza swali la nyongeza ambapo alisema zoezi la uandikishaji wa vitambulisho hivyo limekuwa likiendelea na mpaka sasa hivi ni viongozi pekee ndio waliopata. “Sasa napenda kujua kauli ya serikali kwa sababu vitambulisho hivi vinaweza kutumika kwenye kupigia kura katika Uchaguzi Mkuu ujao. “Je, ni lini serikali itamaliza zoezi hili la uandikishaji wa vitambulisho vipya ili wananchi wote waweze kupata vitambulisho hivi?” alihoji Silinde.

        Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, akijibu swali hilo alikiri kuwa kasi inayotumika kwa ajili ya uandikishaji wa vitambulisho ni tofauti na walivyoitegemea huku akibainisha kwamba jumla ya watu milioni 2.7 wameandikishwa. Hata hivyo, serikali ilipanga zoezi hili limalizike mwakani na vitambulisho hivyo viwe ni sehemu ya mchakato wa kupiga kura na matumizi mengine. “Kweli kuna tatizo…na tatizo hasa lipo kwenye bajeti, mahitaji ya NIDA kwa ajili ya shughuli hii hayafikiwi kwenye bajeti,” alisema.


         Katika swali la msingi, Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman Khalifa (CUF) alitaka kujua kama raia wa nchi nyingine hawawezi kuvipata vitambulisho vya taifa na iwapo zoezi la kuhesabu watu halikuwagusa raia wa kigeni. Naibu waziri alisema: “Ni kweli kuwa nchi yetu imezungukwa na nchi zenye migogoro, hivyo kutoa viashiria vya kuweza kuandikisha watu wasiostahili.” Alisema katika kuhakikisha kuwa hawaandikishi watu wasiohusika, serikali imepeleka madaftari ya wakazi yanayoratibiwa na serikali za mitaa ambayo lengo lake ni kuandikisha wakazi wote wa kila kaya na kuhifadhi taarifa zake.

Source; Tanzania Daima. (June 2013). Mbunge ahoji upatikanaji wa vitambulisho vya taifa. Dodoma. Retrieved from Tanzania Daima

No comments: