Suzan Lyimo, Mbunge CHADEMA. |
Alisema anataarifa ya kufanyika kwa kikao cha Baraza la Mawaziri Novemba 14 mwaka jana na Waziri Dk. Kawambwa alihudhuria katika kikao hicho, ambapo suala la mfumo huo mpya kutumika kupanga matokeo lilizungumzwa. Alidai barua aliyonayo ni kuhusu utaratibu wa matumizi ya alama za maendeleo ya viwango vya ufaulu katika mitihani iliyoandikwa na Kamishna wa Elimu na pia ana barua nyingine ya Desemba 12 iliyoandikwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ikielezea suala hilo. Alisema ingawa Dk. Kawambwa na Lukuvi walikuwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri wakati mfumo huo ukijadiliwa, lakini Lukuvi alipofika bungeni baada ya kikao hicho aliliambia Bunge kuwa wameamua kubadilisha matokeo hayo na sababu kubwa ni kwamba wadau hawakushirikishwa katika utaratibu huo mpya.
“Kama Waziri wa Nchi ambaye ana-represent (anawakilisha) mawazo ya Baraza la Mawaziri amekuja ndani ya Bunge lako tukufu akaeleza kilichojiri na kwanini serikali imeamua kubatilisha matokeo halafu akatoa sababu kubwa kwamba wadau hawakushirikishwa lakini Dk. Kawambwa akasema walishirikishwa” alisema.
Source: Sauwa S. ( June 2013).Mbunge agonganisha kauli za mawaziri. Dodoma. Retrieved from Ippmedia/ Nipashe
No comments:
Post a Comment