Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Thursday, May 30, 2013

‘Tuandamane kupinga muswada wa mabadiliko ya uchaguzi 2015


      Arusha, Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema amewataka wakazi wa Arusha, kujiandaa kwa maandamano hadi bungeni Dodoma, kupinga kuwasilishwa muswada wa mabadiliko ya kufanyika Uchaguzi Mkuu, badala ya 2015 ufanyike 2017.Akizungumza katika mkutano wa kampeni jana katika Kata ya Kaloleni, Lema alisema kuna taarifa kuwa kuna mpango wa kupelekwa bungeni muswada wa mabadiliko ya uchaguzi ujao, jambo ambalo linapaswa kupingwa kwa nguvu zote. “Tunajua wabunge wa CCM wataukubali muswada kwani wanajua ukifanyika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 wengi hawatashinda, lakini wajue nguvu ya umma itashinda,” alisema Lema.
         Lema ambaye kesi yake ya kufanya vurugu Chuo cha Uhasibu Ausha, imepangwa kuanza kusikilizwa Julai 2 baada ya upelelezi kukamilika, alisema kuna hoja kuwa Uchaguzi Mkuu lazima ufanyike baada ya kukamilika kwa mchakato wa Katiba Mpya au kuwapo na fedha za kutosha jambo ambalo Chadema hawatalikubali. “Tunajua mwaka 2015 Chadema tunachukua nchi hivyo, hatutaki kuwaongezea muda CCM na tukichukua nchi tu kama nikichaguliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani katika kipindi cha miezi sita kitaeleweka,” alisema Lema. Alisema ndani ya miezi sita Serikali ya Chadema,itahakikisha fedha zote zilizofichwa Uswisi na nchi nyingine zinarudi na watuhumiwa kufikishwa mahakamani.
       Akizungumzia uchaguzi mdogo wa Kata ya Kaloleni,Themi, Kimandolu na Elerai,Lema alisema chama hicho kina uhakika wa ushindi kwani wagombea wake wanakubalika na wana uwezo. Hata hivyo, aliwataka wakazi wa Kaloleni na kata nyingine, kujitokeza kwa wingi kupiga kura June 16, ili mchana tayari wawe wanashangilia ushindi. Lema alisema wanataarifa za kugawanywa fedha mitaani, akawataka wafuasi wa Chadema kuzichukua fedha hizo kwani ni kodi zao, lakini kura wapige kwa Chadema. Awali mgombea wa udiwani wa Chadema wa kata hiyo, Emanuel Kessy alitoa ahadi kuwa akichaguliwa,atahakikisha wazee wote wanatibiwa bure, hakuna watoto wa shule watakaorudishwa nyumbani kwa kukosa ada pia ataimarisha usafi wa kati hiyo.
        Mgombea wa udiwani wa Kata hiyo kupitia CUF, Abbas Mkindi maarufu kama Darwesh akizungumza katika kampeni juzi hiyo , aliwataka wakazi wa kata hiyo, kutofanya makosa kuchagua watu wasio na uchungu na kata hiyo. “Mimi mnanifahamu hapa, nimezaliwa hapa, tumekuwa wote hapa,na hivyo najua shida zetu naomba mnichaguwe,” alisema Mkindi.
Source: Juma M. (May 2013).  ‘Tuandamane kupinga muswada wa mabadiliko ya uchaguzi 2015’. Arusha. Retrieved from Mwananchi

No comments: