Viongozi kadhaa wa CUF, wamehojiwa na Polisi kutokana na kile kinachodaiwa kuwa chama hicho kinashiriki kuchochea vurugu za Mtwara. Taarifa za kuhojiwa kwa viongozi hao zilithibitishwa Dar es Salaam jana na Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro, wakati akizungumza na wandishi wa habari. Alisema hata hivyo hakuna kiongozi aliyekamatwa, akihusishwa na tuhuma hizo. Alisema viongozi hao walihojiwa wiki iliyopita katika Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam na Mtwara.
“Waliohojiwa ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya CUF Katani Katani na Katibu wa Wilaya ya Mtwara mjini, Said Kulaga,” alisema. Alisema chama hicho kilikuwa na taarifa za kina kuhusu mpango wa kuwakamata viongozi wa ngazi za juu kwa madai ya kuchochea vurugu hizo.
Source: Mhando A. (May 2013).CUF wahojiwa kwa ghasia za Mtwara. Dar. Retrieved from Mwananchi
No comments:
Post a Comment