Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Friday, March 22, 2013

"Serikali iwataje watesji wa Kibanda, Ulimboka"


  









PAMOJA na vyombo vya dola kupiga chenga katika kuwakamata watuhumiwa wa matukio ya kutekwa, kuteswa na kuumizwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Stephen Ulimboka na Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006), Absalom Kibanda, serikali imetakiwa iwataje wahusika na kuwachukulia hatua. Kauli hiyo imetolewa na baadhi ya maofisa wastaafu katika vyombo mbalimbali vya dola, waliozungumza na gazeti hili jana, wakidai kwa sasa vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya kazi kwa shinikizo la kisiasa. Maofisa hao ambao waliomba kuhifadhiwa majina yao, walidai kuwa inashangaza kuona idara nyeti kama ya usalama wa taifa na jeshi la polisi watendaji wake wanatajwa kuhusika katika matukio hayo ya utesaji raia lakini hawakamatwi kuhojiwa na kuchukuliwa hatua. Walisema kuwa badala yake umegeuzwa kuwa mchezo wa kufifisha na kuwahamisha watu kwenye hoja hizo kwa kuibua matukio mengine ambayo yanavaliwa njuga kwa nguvu nyingi pasipo sababu.


Afisa mmoja mstaaafu alitolea mfano suala la kutekwa, kuteswa kwa Dk. Ulimboka akisema kuwa alishangazwa na kauli ya Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema, kudai kwamba suala hi siri ya taifa. “Ninashindwa kuelewa kwa nini polisi au vyombo vyovyote vya usalama havijamkamata wala kumhoji ofisa wa Ikulu, Ramadhan Ighondu, aliyetajwa kuhusika na tukio la Dk. Ulimboka,” alisema. Aliongeza kuwa alichokisema akiwa mahututi hakitofautiani na alichokisema baada ya kupona, lakini akahoji kwa nini polisi hawakuwahi kumhoji Ighondu badala yake serikali ilikimbilia kulifungia gazeti la MwanaHalisi lililoripoti taarifa hiyo. “Huu ni mkakati wa makusudi wa kutopeleleza kitu kinachojulikana, kwani wenye jukumu hili wanawajua watesaji au wanajua sakata lote nyuma ya hili suala ndiyo maana hawapelelezi,” alisema. Ofisa mwingine alidai kuwa matukio hayo likiwemo la Kibanda na mengine yanatoa tafsiri kuwa serikali haiwajibiki.

Alisema watu waache kusingizia kuwa nchi imeharibika, bali inaharibiwa na serikali kwa kutowajibika. Alisema upelelezi matukio ya Ulimboka, Mwangosi na Kibanda unazidi kusuasua huku vyombo hivyo vikiwa vimeibua suala jipya la video ya Wilfred Lwakatare na kuhamisha mjadala wa wananchi.

“Tukio la Mwangosi picha zinaonyesha wazi alivyouawa, lakini pamoja na wale waliomuua kuonekana, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa, na ninyi waandishi mmeacha kuandika, hivyo hivyo suala la Kibanda limenyamaziwa sasa, mnajihusisha na Lwakatare,” alisema ofisa huyo. Usiku wa kuamkia Juni 27, 2012, watu wasiojulikana walimteka kisha kumpiga na kumjeruhi vibaya Dk. Ulimboka. Pamoja na polisi kudai kuunda kamati ya uchunguzi, baadaye walitupiana mpira wakidai hakuna kamati kama hiyo huku Ulimboka mwenyewe kutowahi kuhojiwa hadi leo. Kibanda naye alitekwa na kuteswa Machi 6, mwaka huu, lakini hadi leo hakuna mtuhumiwa aliyekamatwa kuhusika na tukio hilo wakati video ya Lwakatare iliyoonekana mtandaoni Machi 11, polisi wamekwishachunguza na kuwakamata watuhumiwa na kuwafikisha mahakamani. Akizungumzia uharaka huo wa kumkamata kiongozi huyo wa CHADEMA, ofisa maarufu mstaafu wa idara ya usalama wa taifa alidai kuwa suala hilo linapoteza heshima ya serikali kwani sasa inaonekana kulinda wauaji wanaoua wanaharakati au watetezi wengine.

Source: Tanzania daima (March 2013). Serikali iwataje watesji wa Kibanda, Ulimboka. Retrieved from Tanzania Media

No comments: