Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Thursday, March 14, 2013

POLISI YAZUIA MAANDAMANO YA MAJI UBUNGO


Jeshi la Polisi mkoani Dar es Salaam kanda ya Kinondoni limekataza maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika tarehe 16 Machi 2013 yaliyokuwa  yameiratibiwa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika yaliyolenga kufika katika Wizara ya Maji ili kufikisha ujumbe kwa Waziri wa Maji, Prof Maghembe kuhusu kero ya maji katika jimbo hilo ambayo haijatatuliwa wala kupatiwa ufumbuzi kwa muda mrefu. Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo ACP, Charles Kenyela amesema endapo maandamano hayo yatafanyika:
1. Upo wasiwasi wa kutokea kwa vurugu pale watakaposhindwa kufikia muafaka kuhusu hoja zao. 
2. Amewasiliana na Ofisi ya Waziri husika na kufahamishwa kuwa haina taarifa rasmi za ujio wa maandamano hayo. 
3. Barabara yatakakopita maandamano hayo ipo katika ujenzi na hivyo maandamano hayo yatazuia shughuli za mkandarasi kukamilisha kazi yake kwa wakati na kuisababishia Serikali hasara. 
4. Eneo ambamo maandamano hayo yanakusudiwa kutamatia ni dogo na hivyo itasababisha usumbufu mkubwa.

Source: Wavuti. (March 14, 2013). Polisi yazuia maandamano ya maji Ubungo. Retrieved from Wavuti

No comments: