Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Thursday, March 14, 2013

KUKAMATWA KWA LWAKATWARE CHADEMA YAFAFANUA, CCM NA USALAMA WA TAIFA WAHUSIKA WAKUU




CHADEMA YAZUNGUMZIA KUKAMATWA KWA LWAKATWARE

Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk Slaa amezungumza na wanahabari (video imepachikwa hapo chini) kuhusiana na tukio la jana la kiongozi mmoja wa chama hicho, Wilfred Lwakatware kuwekwa chini ya ulinzi wa Polisi tokea jana kwa ajili ya mahojiano ya kiuchunguzi. Slaa akasema CHADEMA inalitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wake kuhusiana na suala hilo bila kufuata mrengo wa kisiasa. Slaa pia amesema CHADEMA inashangazwa na hatua iliyochukuliwa na Jeshi hilo kumkamata Lwakatare kwa kuona video il hali zikiwapo taarifa nyingi za uchochezi ambazo wasemaji wake hawajachukuliwa hatua. Akasema haamini kama Lwakatare anaweza kupanga mipango ya kufanya uvunjifu wa amani. Pia amesema kwa muda mrefu wamekuwa wakipeleka malalamiko yao na vielelezo mbalimbali polisi kuhusu kuhujumiwa lakini hadi sasa hakuna uchunguzi uliofanywa na Jeshi hilo.


Source: Wavuti. (March 14, 2013). CHADEMA yazungumzia kukamatwa kwa Lwakatware. Retrieved from Wavuti

No comments: