Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Sunday, March 31, 2013

Kigogo wa CCM Ngara adaiwa kuunda genge la mauaji


Wakazi wa kijiji cha Omukagando wilayani Kyerwa mkoani Kagera wamemtuhumu kiongozi mmoja wa kijiji hicho (jina linahifadhiwa) kuunda kikundi cha mauaji cha "Hakuna kulala" ambacho mpaka sasa kidaiwa kufanya mauaji ya watu sita. Akieleza hofu ya wanakijiji hao, Ofisa Mtendaji wa kata ya Mabira, Herman Leonard, alisema wasiwasi wa mauaji hayo umeongezeka baada ya kijiji hicho kuandamwa na matukio mfululizo ya mauaji yanayodaiwa kufanywa na kundi hilo kwa lengo la kukamata, kupiga na kuwaua wahalifu. Alisema kiongozi huyo anatuhumiwa kuhusika na kipigo na vifo vya ndugu wawili waliodaiwa kuteswa na kuuawa na wana ‘hakuna kulala’ wakidaiwa walimuua mtoto wa kiongozi huyo. Herman alisema mwanzoni mwa mwezi huu alipigiwa simu na mtu aliyeficha namba akimweleza kuwa watuhumiwa waliokuwa wakitafutwa wamepatikana, lakini alimuagiza mpiga simu kuwaleta kwake ili kuwafikisha kituo cha polisi.

Hata hivyo, alisema baadaye jioni alimuona kiongozi huyo anayetuhumiwa kuanzisha kundi la mauaji akiwa amepakiza watu ndani ya gari yake wakiwamo watuhumiwa wawili waliodaiwa kukamatwa ambao ni Danes Damian (34) na Johnson Damian (37) waliokuwa mahututi. "Kwakweli walikuwa hoi, nilimwomba kiongozi huyo awapeleke kituo cha afya kwanza wapatiwe huduma ya kwanza “, alisema Herman na kuongeza kuwa kutokana na kuwa na mashaka juu ya watuhumiwa hao kufikishwa alikoelekeza, iliwaamuru mgambo kufuatana nao. Alisema mgambo waliwasindikiza mpaka kwa Mkuu wa Polisi wa Nkwenda (OCS) ambaye naye alimwamuru kiongozi huyo kutoka chama cha siasa kwenye kata kuwapeleka kituo cha afya cha Nkwenda ili wapatiwe huduma kutokana hali mbaya. Baada ya watuhumiwa kufikishwa katika kituo cha afya Nkwenda, ilibainika kuwa majeruhi Danes Damian alikuwa amefariki lakini Johnson Damian alikuwa hai licha ya kuwa mahututi jambo lililomlazimu kiongozi huyo kukimbia.

Ofisa mtendaji huyo alikiri kuwepo matukio ya vifo vinavyotokana na kipigo katika kata hiyo, jambo linahusishwa na kikundi cha ‘hakuna kulala’ kilichokuwapo miaka miwili iliyopita na kuiomba serikali kuongeza kituo kingine cha polisi, kutoa elimu ya haki za uraia ili kuisadia jamii ya hapa.Herman alisema marehemu hao wote walikuwa viongozi wa TLP katika kitongoji cha Nyakatete ambapo Danes alikuwa Mwenyekiti Johnson ni Katibu . Kamugisha Damian (30) mdogo wa marehemu Danes, akieleza tukio hilo alisema alikuwa shuhuda wa mateso waliyoyapata marehemu wawili, kwani siku hiyo alikuwa na kaka zake shambani eneo la Kashanda-Akibira wakilima viazi na kuvamiwa na kundi la watu likiwa na kiongozi wa chama na kuwaamuru kaka zake (marehemu) kujisalimisha kwani wako chini ya ulinzi . Alisema aliamrishwa kulala kifudifudi na kutochungulia lililotokea kwa ndugu zake, amri iliyokuwa ikitolewa na kiongozi huyo aliyemwelekezea bunduki. Alisimulia kuwa kabla ya ndugu zake kukamatwa na kufungwa kamba kupelekwa porini, kigogo huyo alianza kumtishia kuwa endapo atamfuatilia atammaliza kwa kumpiga risasi, jambo ambalo ilimbidi kuwa mpole huku akishuhudia wenzake wakipigwa na kupelekwa porini.

Alisema kijijini hapo hofu imetanda kutokana na hofu juu ya kiongozi huyo kukamata watu na kuwapiga ikizingatiwa anamiliki bunduki lakini wananchi wakilalamika kwanini serikali inashindwa kumchukulia hatua za kisheria.
Mganga Mkuu Msaidizi wa kituo cha Afya Nkwenda, aliyechunguza majeruhi waliofikishwa kupatiwa matibabu Dk.Pontian Masinde, alithibitisha vifo vya Johnson Damian na Danes Damian, ambao walifikishwa kituoni hapo siku ya tukio na kigogo huyo wa chama alimtaja kwa jina. "Mheshimiwa alifika saa 6 usiku akidai ana majeruhi ndani ya gari lake lililokuwa limebaki nje ya kituo, aliniomba nikawaone ndani kuwapatia huduma kwa madai walikuwa wameteswa kidogo nilikataa nikamwambia awalete niwapime, " alisema. Dk.Masinde alisema baada ya kumpima wa kwanza aligundua kuwa amefariki na wa pili alikuwa hoi na kupoteza damu nyingi kisha kumpa kigogo huyo taarifa ambapo alitoroka, licha ya kumwambia polisi aliyekuja naye kuwa mheshimiwa anamtoroka. Alisema kundi lake lilimpeleka majeruhi katika hospitali teule ya wilaya ya Nyakahanga ambapo alipoteza maisha pia. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Philip Kalangi, alithibitisha kupokea taarifa juu ya kuwapo mauaji hayo yaliyofanywa na kigogo huyo ambaye ametoroka na msako unaendelea. Awali ilidaiwa ametorokea nchini Uganda na kuacha familia kijijini. Mtuhumiwa hakupatikana kujibu tuhuma hizo.

Source: Nipashe/Ippmedia (March 2013). Kigogo wa CCM Ngara adaiwa kuunda genge la mauaji. Retrieved from Ippmedia/Nipashe

No comments: