Dar es Salaam. Diwani wa Kata ya Mwanga Kusini kupitia CCM mkoani Kigoma, Anord Mtewele, amemlaumu Katibu wa CCM Mkoa wa Kigoma, Mohamed Nyawenga akidai alimshambulia na kumdhalilisha kwa kumpiga na kumtolea lugha chafu. Mtewele alisema bosi wake huyo alimtendea hayo siku ya Jumapili iliyopita mchana akiwa kwenye gereji iliyoko Mwanga Kaskazini ambako gari lake lilikuwa likikarabatiwa.“.Katibu wa CCM mkoani Kigoma Nyawenga alipoulizwa kwa simu na gazeti hili alionyesha kushangaa juu ya suala hilo huku akisema hajawahi kulifanya. “Kwanza nakushangaa kusema nilimshambulia na kumpiga, wala sijawahi kumwona na hata mimi"
Source: Majura E. (March 6, 2013). katibu wa CCM adaiwa kumpiga diwani wa Mwanga. Retrieved from Mwananchi
No comments:
Post a Comment