Jukwaa la Katiba Tanzania limeshauri kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ichaguliwe na wananchi pamoja na vyama vya siasa baada ya kwa kupitishwa kwa sheria bungeni ya tume huru ya uchaguzi na mipaka ili kuepusha manung’uniko kutoka kwa wagombea baada ya matokeo kutangazwa. Kadhalika Jukwaa hilo limesema kuwa Uchaguzi Mkuu wa urais ufanyike siku za kazi na kupendekeza kuwapo kwa sheria ya kuzitaka ofisi zote na maduka kufungwa ili kuwezesha watu kutumia haki yao ya msingi ya kupiga kura kama ilivyofanyika katika Uchaguzi Mkuu nchini Kenya wili iliyopita. Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mjumbe na Jukwaa la Katiba, Hebron Mwakagenda, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Deus Kibamba, alipokutana na waandishi wa habari.
Alisema Jukwaa la Katiba lilikwenda Kenya kuangalia mchakato wa uchaguzi chini katiba mpya kwa kutembelea ofisi za msajili wa vyama vya siasa, Tume Huru ya Hchaguzi na Mipaka (IEBC), Tume ya utekelezaji wa Katiba (CIC) na vituo vya kupigia, kuhesabia na kukusanya kura. Alisema serikali inapaswa kujifunza kutoka katika uchaguzi wa Kenya kwa kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi na mipaka kwa kupitishwa kwa sheria bungeni na kuridhiwa na vyama vyote vya siasa itakayoendesha ma kusimamia chaguzi zote zilizopo kikatiba na sheria.
Source: Mfuru J (March 2013). Jukwaa la katiba lataka tume huru ya uchaguzi. Retrieved from Ippmedia/Nipashe
No comments:
Post a Comment